HABARI ZAIDI KUHUSU KIJANA ALIYEUAWA KWENYE FIESTA SHINYANGA

Mwili wa marehemu Musa Shija mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa mtaa wa Mwalugoye kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga aliyeuawa kwa kushambuliwa akiwa kwenye Fiesta usiku wa kuamkia leo katika uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza na Malunde1 blog mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema uchunguzi  wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.



Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mussa Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kijana huyo aliuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana nje ya fensi la uwanja mdogo wa Kambarage palipokuwa panafanyika tamasha la Fiesta.

Hata hivyo amesema jeshi la polisi litatoa taarifa kamili baadaye kwani linaendelea kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha tukio 

Na Kadama Malunde-Shinyanga

Endelea kutembelea blog hii kwani malunde1 blog inaendelea kufuatilia tukio hili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post