HABARI MPYA

Rss

Saturday, April 19, 2014
no image

WANAOPUUZA WAASISI WA TAIFA WANA KANSA YA UBONGO

Wananchi wa kijiji cha Mwamashimba kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamesikitishwa na vitendo vya baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba vya kutukana na kudhihaki waasisi wa taifa na kudai kuwa watu hao  wanaokashfu viongozi huenda wana ugonjwa wa kansa ya ubongo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho,wananchi hao walisema vitendo vya kuwakosea heshima waasisi wa taifa akiwemo baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hayati Amani Abeid Karume siyo vya kiungwana kwani viongozi hao ndiyo waliolifikisha taifa hapa lilipo.

Walisema kumekuwa na tabia ambazo siyo za kiungwana tena kinyume na maadili ya kitanzania zinazofanywa na baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba kama vile kudhihaki kazi waliyofanya waasisi hao kuunganisha nchi mbili Tanganyika na Zanzibar.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Shija Manoni alisema waasisi hao walifanya kitu kizuri cha kuunganisha nchi mbili kutokana na upeo na ulewa wao na kwamba kama kuna mapungufu basi wangetumia ufahamu na elimu zao kutatua changamoto za muungano lakini siyo kuuvunja.

“Ndugu waandishi,unajua kwa mtu mwenye akili timamu kuwapuuza waasisi wa taifa, ni laana kubwa,waasisi hawa ndiyo waliosababisha tuishi kwa mshikamano,upendo na amani,na ndiyo walisababisha hata hawa wanaojiita wasomi kupata kupata elimu wanayayojivunia”,aliongeza Manoni.

Kwa upande wake bi Malimi John mkazi wa kijiji hicho mwenye umri wa miaka 68 aliyekuwa akiongea kwa shida kwa lugha ya kisukuma alisema watu wasiojua kusoma walidai uhuru na waasisi wa taifa,na baada ya kupata uhuru walijiwekea mikakati ya kusomesha watoto ili waje kuwa wataalamu kuisaidia nchi na matokeo yake wasomi hao wameanza kutukana wazee.

“Sisi tunashangaa kusikia wasomi wetu wanadharau waasisi wa taifa hadi baba wa taifa,wakati sisi tunamweshimu alitutoa mikononi mwa wakoloni,tukawa kitu kimoja,hivi hawa wana akili timamu kweli,au wana matatizo ya kansa ya ubongo?”,alihoji mama huyo.

Bi John alisema ni vyema wajumbe wa bunge la katiba wakatumia elimu yao kutatua changamoto za muungano badala ya kuanzisha ujanja ujanja wa kuvunja muungano kwani muungano ndiyo umelifikisha taifa hapa lilipo.

via>>Zanzibar Leo
UNAFIKIRI NANI ATAWATETEA HAWA?? WANANYANYASIKA KILA KUKICHA

UNAFIKIRI NANI ATAWATETEA HAWA?? WANANYANYASIKA KILA KUKICHA


Bado maeneo ya mikoa ya Shinynga na Simiyu imeonekana kuwa wakazi wake wana tabia ya kuwanyanyasa wanyama kama inavyojieleza katika picha ambapo kamera za mtandao huu wa malunde1 blog ziliwanasa wanyama hawa aina ya punda wakiwa wamebebeshwa mizigo mizito zikiwemo injini za gari,matairi na vyuma mbalimbali kinyume na taratibu za haki za wanyama katika kijiji cha Wigelekelo wilaya ya Maswa mkoa mpya wa Simiyu.


Wanyama wameendelea kunyanyaswa wakati asasi nyingi za kutetea haki za wanyama kama vile Tanzania Animals Pritection Organisation (TAPO)yenye makao yake jijini Dar es salaam na ofisi yake iliyopo Kahama mkoani Shinyanga na wahusika wengine wengi wakiwa wamekaa kimya. Ng'ombe,mbwa,punda,paka na hata ndege wafugwao wamekuwa wakinyanyasika kwa kupigwa,kutopata huduma za afya,kubebeshwa mizigo mizito,kutopewa chakula.


Je ni nani atakayewatetea wanyama hawa!??
Friday, April 18, 2014
no image

KUHUSU MASAI NYOTAMBOFU KUJIONDOA KWENYE KUNDI LA VICHEKESHO LA VITUKO SHOW

MCHEKESHAJI maarufu hapa nchini katika swaga za kimasai ambaye pia ni mmiliki wa masainyotambofu.info Gilliady Severine Kahema 'Masai Nyotambofu' Ameamua kuitema kampuni aliyokuwa na mkataba nayo ya Al-Riyamy Pro ambayo hurusha kipindi chake cha VITUKO SHOW kwenye runinga ya CHANNEL TEN.  

no image

RAIS MUGABE ATISHIA KUWAFUKUZA NCHINI KWAKE WANAOPIGIA DEBE USHOGA,ALIWAHI KUWATAJA MASHOGA KUWA WABAYA KULIKO MBWA NA NGURUWE

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ametishia kuwafukuza kutoka nchini humo wanadiplomasia wanaopigia debe mapenzi ya jinsia moja.

Katika hotuba yake ya sherehe za kuadhimisha uhuru wa nchi hiyo, Mugabe alitumia fursa hiyo, kukaripia kile alichokiita upuuzi wa nchi za ulaya zinazohubiri ushoga.

Alituhumu nchi za ulaya kwa kukosa maadili na kusisitiza kuwa ndoa inaweza kuwa tu kati ya mwanamke na mwanamume.

Sio mara ya kwanza Mugabe amekemea suala la ushoga.
Aliwahi kuwataja mashoga kuwa wabaya kuliko Mbwa na Nguruwe.

Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Zimbabwe na mashoga hukamatwa mara kwa mara kwa kosa hilo
via>>bbc
no image

MELI YAZAMA KATIKA ZIWA VICTORIA IKITOKEA BUKOBA KWENDA MWANZA

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Meli ya mizigo ya Kampuni ya FB Matara iliyokuwa inatoka Bukoba kwenda Mwanza ikiwa na wafanyakazi kumi na shehena ya sukari imezama ziwa victoria katikati ya visiwa vya Kerebe na Bumbile.
Habari kamili itakuja hivi punde endelea kutembelea mtandao huu
no image

TAZAMA HAPA VIDEO YA RAIS KIKWETE AKIZUNGUMZIA WATU WANAOWASEMA VIBAYA WAASISI WA TAIFA,ASEMA VITENDO HIVYO NI KUKOSA ADABU TU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongelea wanaowasema vibaya waasisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Abeid Aman Karume na Julius Kambarage Nyerere wakati wa mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es salaam Aprili 15, 2014.

TAZAMA HAPA CHINI VIDEO RAIS KIKWETE AKIZUNGUMZA

SIKILIZA NA PAKUA MUZIKI HAPA

Copyright © 2014 MALUNDE All Right Reserved
Designed by HAROLD.