Hii Nayo Kali!! WAJANE WAWILI WAUAWA KWA KUDAIWA KUENEZA KIPINDUPINDU KISHIRIKINA HUKO MBEYA






Wajane wawili wa Kitongoji cha Bulinda wilayani Kyela wameuawa kwa mapanga wakidaiwa kusambaza ugonjwa wa kipindupindu baada ya kufiwa na waume zao katika eneo hilo.


Waliouawa ni Geneli Kapwela (65) na Rahabu Bungulu (70) waliokuwa wakiishi peke yao.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema jana kuwa wajane hao waliuawa juzi baada ya kipindupindu kuhusishwa na imani za kishirikina.


Takwimu za mauaji toka polisi zinaonyesha karibu watu wawili wanauawa mkoani Mbeya kwa imani za kishirikina

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527