Angalia Picha!! HUYU NDIYO MSHINDI SHINDANO LA MISS ALBINISM KANDA YA ZIWA


Miss Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshindi katika Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.


Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.

Mrimbwende Zawadi Dotto (Pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.



Wshiriki Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17), Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18), Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.



Washiriki walioingia Nne bora ambapo kutoka kushoto Hajra Sadru, Furaha Edward, Zabibu Abdallah na Zawadi Dotto



Baada ya Mtifuano mkali hatimae majaji wakatangaza washini. Furaha Edward mshindi wa tatu (Kushoto), Hajru Sadru mshindi wa pili (katikati) na Zawadi Dotto akaibuka kuwa mshindi wa Kwanza (aliepiga magoti).



Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.



Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.



Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu



Kampuni ya Visimbuzi (Ving'amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick Makonya ambae ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja zawadi zilizotolewa kwa washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa Kwanza amejinyakulia Simu ya StarTimes aina ya Solar5, Mshindi wa Pili simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.



Baadhi ya Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi.



Alexander Exaud Mutowo ambae ni Mratibu wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION lililoandaa mashindano hayo akizungumza wakati wa mashindano hayo, ambapo amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwemo kuunga mkono juhudi za shirika hilo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jiko katika katika kituo cha kuwahifadhi watu wenye ulemavu wa ngozi Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga.



Fredy Samwel Kaula ambae ni Mwenyekiti wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION akizungumza katika Mashindano hayo



Alfredy Kapole ambaye ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS akizungumza wakati wa mashindano hayo



Mwenye kinasa sauti ni Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, akifungua mashindano hayo. 

Amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza itaendeleza ushirikiano na Shirika la VUNERABLE FOUNDATION kwa ajili ya kupata wadau wa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi.



Dickson Kiringo a.k.a Mr.White ambae ni Msanii chipukizi wa Muziki wa Kizazi kipya akitoa burudani. Msanii Barnaba Boy aliahidi kumsaidia Mr.White ili arekodi nyimbo mbili katika studio yake ikiwa ni bure kabisa.



Msanii Barnaba Boy akitoa burudani katika shindano la Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.



Majaji ambapo kutoka Kushoto ni Jaji Angelina Chuma, Jaji Mkuu Jalia Mtani na Jaji Lilian Lambo



Wa pili kulia ni Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS pamoja na wadu wengine wakifuatilia mashindano hayo



Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa BINAGI MEDIA GROUP

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527