MSIBA WA KIGOGO WA CHADEMA ALIYEUAWA GEITA WAZIDI KUZUA BALAA




Baada ya zoezi la kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo kushindikana kutokana na jeshi la polisi mkoani Mwanza kupiga marufuku mikusanyiko ya wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa madai ya kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Mwanza, hatimaye viongozi wakuu wa kitaifa wa Chadema pamoja na familia ya marehemu wameamua kwenda mahakamani kutafuta haki yao ya kisheria. 



Mwenyekiti wa Chadema taifa Mh. Freeman Mbowe anajitokeza mbele ya waandishi wa habari na wabunge 45 wa kambi ya upinzani kutoa msimamo wa chama hicho baada ya vikao vya mashauriano. 


"Tumekubaliana kuahirisha  mazishi yalikuwa yamekusudiwa na kulazimika kwenda kutafuta mahakamani kama chama kinachojenga demokrasia kwani kama hatutendewi haki na chombo chochote cha dola basi tunatafuta haki mahakamani",amesema Mbowe.

Waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye pamoja na aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Mh. Edward Lowassa nao wametoa angalizo kwa jeshi la polisi nchini. 


"Hatujawahi serikali  inakataza wananchi wao kuzika ndugu yao ..watu hawa hawana silaha,watu hawa wanataka kumzika kwa heshimu...Chadema na familia watakuwa watu wa mwisho kuona fujo inatokea mwili wa Mawazo uko hapo...haya mambo wanayoyafanya wao ndiyo wanaweza kusababisha fujo",amesema Sumaye.






"Wao ndiyo wamechokoza fujo...sisi tunajiheshimu...hatuna nia ya kufanya fujo,tunataka kumzika ndugu yetu",amesema Lowassa.


Mchungaji Charles Lugiko ni baba wa marehemu Alphonce Mawazo amesema ameumizwa na kitendo cha askari polisi kwenda hadi nyumbani kwake eneo la Nyegezi na kuwatawanya waombolezaji.

Alphonce Mawazo aliuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika kijiji cha Katoro wilayani Geita.


Via>>Itv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527