Maskini !! MMOJA KATI YA WATANO WALIOISHI KWA KULA MENDE NA VYURA MGODINI KAHAMA AFARIKI DUNIA



Mhanga mmoja kati ya watano wa ajali ya mgodi wa dhahabu wa Nyangalata waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia.. 



Akithibitisha kifo cha mtu huyo mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dr.Joseph Ngowi amesema hadi jana usiku afya ya mgonjwa huyo ilikuwa nzuri lakini leo asubuhi alianza kutapika mfululizo na ilipofika  leo saa sita mchana akafariki dunia.

Nao baadhi ya ndugu wa marehemu wamesema wamepokea kifo cha ndugu ya kwa masikitiko lakini wanamshukuru mwenyezi mungu na sasa wanajiandaa kuusafirisha mwili wa ndugu yao kwenda nyumbani kwao Tarime kwa ajili ya mazishi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Vitta Kawawa amesema halmashuri yake imepokea taarifa za kifo hicho kwa masikitiko kwa kuwa walikuwa wanafanya jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapona na kurejea katika familia zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527