KATIBU MKUU KIONGOZI TANZANIA AFANYA ZIARA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUKAGUA VITANDA VYA RAIS MAGUFULI




Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue leo amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.

 Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema amekagua mashine za MRI na CT-SCAN na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea.

Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.

 Pia, amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.

 Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya Tehama na kuwa na maduka yao ya ndani.

Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando na watendaji wa MNH ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527