JINSI WABUNGE WA UKAWA WALIVYOAMRIWA KUTOKA BUNGENI WALIPOANZA KUZOMEA,ZITTO KABWE ABAKIA,AFUNGUKA


Wabunge wanaounga umoja wa Katiba Ya Wananchi, UKAWA wametolewa nje ya ukumbi wa bunge muda huu baada ya kugoma kutambua ujio wa Dr Shein bungeni na kuanza kuzomea huku wakisema Maalim Seif....Maalim Seif


Wabunge hao awali walitoa msimamo wao wa kutokubali Dk Ali Shein kuhudhuria Bunge hilo wakati rais atakapoingia Bungeni kulihutubia Bunge kwa kuwa hawamtambui kama rais wa Zanzibar kwani kwa mujibu wa Katiba muda wake umekwisha.

Kelele za zomeazomea ziliibuka ghafla wakati Rais Dk Shein alipoingia bungeni hali iliyoondoa utulivu wa Bunge.

Hata hivyo, Mbunge pekee wa upinzani, Zitto Kabwe (ACT – Wazalendo) alibaki ndani ya Bunge kwa utulivu na kuendelea kusikiliza hotuba ya Rais.

Awali, wabunge hao walimuandikia barua Spika wa Bunge wakihoji uhalali wa hotuba ya Rais bungeni endapo Dk Shein atahudhuria Bunge hilo kama Rais wa Zanzibar.

Ukawa wameendelea kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (NEC) kumtangaza mshindi wa nafasi ya Urais wa Zanzibar, huku mgombea wa CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akidai kuwa ameshinda kutokana na kura halali alizokusanya kwenye vituo vyote. 



Spika wa bunge,Job Ndugai aliwataka wabunge hao waache kuzomea na badala yake wakae chini lakini wakakaidi, hali iliyomfanya awaamuru watoke nje kwa hiari yao kabla nguvu ya dola haijatumika kuwatoa.

Hata hivyo Zitto Kabwe amesema kitendo kilichofanywa na wabunge wa Ukawa ni cha kawaida kwani kuna mabunge mengine duniani huwa wanapigana hivyo hiyo ni kuonesha kuwa hawakubaliani na ndivyo demokrasia ilivyo..

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527