Kilichojiri Bungeni!! UKAWA WATOLEWA NJE YA BUNGE,RAIS MAGUFULI AHUTUBIA,HOTUBA YAKE IKO HAPA,BUNGE LAAHIRISHWA HADI TAREHE 26.01.2016



Rais Magufuli leo amehutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma ambapo pia ametoa mwelekeo wa Serikali yake ya Awamu ya Tano katika miaka mitano ijayo.

 Haya ndiyo yaliyojiri..Fuatilia hapa Mwanzo hadi Mwisho
 

Kabla ya kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge, Rais amekagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili


Awali, kabla ya Rais Magufuli kuingia Bungeni,Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alitoa hoja ya kutengua kanuni ili kuwaruhusu viongozi wa kitaifa kuingia bungeni kushuhudia Rais Magufuli akihutubia Bunge.


Tundu Lissu: Napenda tupate muongozo kuhusu baadhi ya wageni kuwakaribisha ndani, kwa hali ilivyo leo hatuna Rais wa Zanzibar, hatuna makamu wa kwanza au wa pili halali wa Zanzibar, hatuna spika wala baraza la wawakilishi Zanzibar.


Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar muda wa serikali ya Zanzibar uliisha tangu Novemba 2.


Naibu spika amemjibu kwa kusema kifungu pia kinasema Rais wa Zanzibar anafikia ukomo mpaka Rais mpya anapoapishwa.

Updates
Muda huu Rais wa Zanzibar ndo anaingia Bungeni,lakini kuna hali ya vurugu. Wabunge wa Ukawa wanazomea huku wakisema Maalim Seif...... Maalim Seif........Maalim Seif.......Maalim Seif


--> Wabunge wa CCM nao wanashangilia huku wakisema CCM......CCM....CCM


Baada ya Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kuingia bungeni,kelele nyingi zinasikika kutoka kwa wabunge wa UKAWA wakipinga kutomtambua huku wakilitaja jina la Maalim Seif.


Kelele za wabunge zinaimba "Maalif Seif, Maalim Seif, Maalim Seif, Maalim Seif..." Lakini taratibu zinaendelea.

Spika wa Bunge Job Ndugai amewaamuru wabunge wanaopiga kelele watoke nje ,wabunge wote waliokuwa wakipiga kelele wametoka nje.


Updates:
Rais Magufuli ameanza kuhutubia bunge

-Anasisitiza kutimiza ahadi zake alizoahidi
-Analipongeza jeshi la polisi na Tume ya Uchaguzi kwa kufanikisha zoezi zima la uchaguzi


-Kampongeza sana Zitto Kabwe kwa kutozomea na kutoka nje kama walivyofanya wabunge wengine wa upinzani


-Rais Magufuli anawapongeza marais wastaafu waliomtangulia kwa nzuri walizofanya


-Kasema tumemaliza uchaguzi tukiwa wamoja, hivyo serikali yake itahakikisha inadumisha amani hii kwa gharama yoyote


-Rais amesema wakati wa kampeni, wananchi walitoa malalamiko mengi kama Rushwa,migogoro ya ardhi,kuhodhi maeneo bila kuendelezwa,uvivu, matumizi mabaya ya mali za umma, matatizo ya maji


-Kasema eneo lingine lililolalamikiwa ni Uwepo wa Rushwa TRA na ukwepaji kodi, Tanesco kukata umeme hovyo, watumishi wa maliasili kujihusisha na ujangili


-Mengine yaliyolalamika ni ubovu wa huduma za afya, lugha chafu za waaguzi na tozo za ajabu


==>Mh.Spika nimeamua kuyataja haya ili tujue pakuanzia


-Sehemu nyingine inayolalamikwa ni uhamiaji, pia suala la Elimu ambapo kuna malalamiko ya walimu na huduma mbovu kwa wanafunzi

-Lawama pia zilitolewa katika sekta ya madini ambapo wazawa hawanufaiki,Mizani rushwa imekithiri,Mahakamani haki zinapindishwa, uvuvib haramu, wakulima kutopewa pembejeo za kilimo


-Eneo lingine ni uchakavu wa Reli, kuzorota kwa shirika la ndege


==> Hizi ni baadhi ya kero ambazo nimezitaja ili kwa pamoja tusaidiane kuzitafutia ufumbuzi


Pamoja na kero hizo, kuna mambo mengine ambayo tumejipanga kuyasimamia na kuyatatua. Mambo hayo ni;


1. Kuulinda muungano wetu
2. Kumarisha mihimiri ya Serikali
-Tumejipanga mihimiri yetu ya Bunge na Mahakama inapata pesa za kujitosha ili iweze kufanya kazi zake kwa uhuru


3. Mchakato wa katiba mpya.
-Serikali yangu inatambua kazi kubwa iliyofanywa na watangulizi wetu pamoja na bunge la katiba lililotupatia katiba pendekezwa.Tunaahidi kutimiza wajibu wetu kumalizia kiporo hiki tulichoachiwa


4.Uchumi na matarajio ya wananchi
-Tutaboresha miundo mbinu ili kuinua uchumi. Tumejipanga kuzijenga upya Reli zetu ili kuboost vizuri uchumi wetu
-Tuna gesi na madini,tutahakikisha wananchi wote wananufaika na rasrimali hizi.


5.Ujenzi wa Viwanda
-Serikali ya awamu ya tano itaweka kipaumbele katika ujenzi wa viwanda
-Tutaanza na Viwanda Vilivyopo na kuhakikisha vinafanya kazi
-Waliobinafishwa viwanda hivyo nawataka waanze kazi mara moja.Wakishindwa tutawanyang'anya mara moja
- Tumejipanga kuhimiza na kushawishi wawekezaji kuwekeza zaidi nchini ili kukuza zaidi uchumi wetu


Sura Ya Viwanda Tunavyotaka Kuviunda
-Sura Ya Kwanza: Ni vile ambavyo malighafi yake itatoka ndani ya nchi

-Sura Ya Pili ya Viwanda hivi ni vile vya kuzalisha vifaa ambavyo vitatumiwa zaidi ndani ya nchi


***Viwanda hivi vitakuwa na uhakika wa soko ndani ya nchi


-Sura Ya Tatu ya Viwanda hivi ni kuzalisha ajira nyingi kwa watanzania


6. Kilimo, Mifugo na Uvuvi
-Tutaziangalia sekta hizi kwa mtazamo wa kibiashara ili kukuza viwanda vyetu.
-Tutahakikisha wavuvi hawavamiwi na majambazi
-Tutafuta kodi za wakulima ambazo hazina ulazima
-Wanachi hawatanyang'anywa ardhi zao kiubabe

7.Umasiki na Ajira
-Nakiri,pengo la wenye nacho na wasio nacho linazidi kuwa kubwa.
-Tumejipanga kupunguza umasikini na kukuza ajira kwa kutilia mkazo uanzishwaji wa viwanda, uvuvi, mifugo na kilimo kama nilivyosema
-Tumejipanga pia kuwawezesha vijana kwa kuwaandaa kielimu na kiujuzi
-Tutahakikisha vyuo vyetu vinawaandaa vijana kiufundi
-Tutawapa vijana mitaji ya kuanzisha kampuni kulingana na fani zao
-Vijana wataanzisha saccos zao na watatakiwa kujiunga na mifuko ya jamii

==> Makundi maalumu ya Bodaboda,mamalishe na Machinga
- Ushuru usio wa lazima kwa machinga, mama lishe tutaufuta
-Nawataka viongozi wote wa halimashauri wasiwanyanyase watu hawa kwa namna yoyote ile na sitawavumila.




8. Afya
-Tutaimarisha huduma za afya pale zilipo na kuzianzisha pale ambapo hazipo
-Tutawapatia mafunzo watumishi wake ndani na nchi
-Tutawapatia vifaa vya kutosha ili kuondoa ulazima wa watu kutibiwa nje
-Tutaongeza bajeti ya wiraza ya afya.

9. Elimu
-Tutaongeza mkazo katika masomo ya sayansi
-Tutahakikisha vifaa na maabara zinaongezwa
-Kuanzia Mwakani elimu ya shule ya msingi hadi kidato cha nne ni Bure
-Wanafunzi wa Vyuo watapata mikopo kwa wakati
-Matatizo ya walimu yatatiliwa mkazo

10. Maji
-Tutaongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 85 vijini na 95 mijini.
-Hatutaki akina mama kubeba ndoo kichwani.Tutaboresha miundo mbinu ya maji

11.Umeme
-Tutakamilisha miradi iliyopo na mingine mipya itajengwa ili kuhakikisha upatikaji wa umeme kwa kiwango kikubwa.
-Pale mtera kuna hujuma, watu wanafungulia maji ili yamwagike hovyo wauze mafuta. Naahidi kupambana Nao.

12.Madawa ya Kulevya.
-Tunaahidi kuusaka kwa gharama zote mtandao wa wauza madawa ya kulevyo.
-Tutashughulika na wakubwa,sio vidagaa na hatutawaogopa na mungu anisaidie

13. Rushwa na Ufisadi.
-Nachukia sana Rushwa na ufisadi
-CCM tumejengwa katika imani ya kukataa Rushwa na Ufisadi, japo sina imani sana kama wanachama wa sasa hawatoi na kupokea rushwa.
-Wananchi wamechoka sana na Rushwa na hawako tayari kuvumilia UPUUZI wa serikali kuwavumilia mafisadi na wala Rushwa
-Dawa ya jipu ni KULITUMBUA......Nimejipa hii kazi ya kuyatumbua haya majipu
-Nafahamu ugumu wa vita niliyoamua kupambana nayo maana Rushwa hutendwa na viongozi wakubwa wa nchi, lakini naamini wananchi wataniunga mkono katika mapambano haya ya Rushwa na Ufisadi.
-Ili kulitatua tatizo hili, nimedhamiria kuanzisha mahakama ya Rushwa na Mafisadi
- Kiongozi yeyote ntakaye mteua na kujihusisha na Rushwa NITAMTIMUA MARA MOJA na hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa

14. Baraza dogo la Mawaziri
-Nimejipanga kuunda serikali ndogo itakayojikta kuwatumika wananchi.
-Watumishi wavivu, wazembe hawatakuwa na nafasi ndani ya serikali yangu
-Tumewavumilia vya kutosha.....Sasa Inatosha, hatutawafumbia macho
-Pamoja na hilo, lakini pia tumejipanga kupunguza kodi ya wafanyakazi na kuboresha mishahara yao.

15.Ukusanyaji wa Mapato na kubana matumizi
-Tumejipanga kushughulika na wakwepa kodi wote ili kukuza uchumi wetu
-Safari zote za nchi tutazifuta na tumeshaanza.
-Hata kama ikitokea kiongozi akasafiri hatutaruhusu aambatane na msafara mkubwa usio na ulazima.
-Takwimu nilizonazo ni kuwa kwa mwaka huu wa pesa zaidi ya bilioni 356.324 zilitumika kwa safari za nje.Huu ni ubadhilifu wa mali za umma
-Warsha,semina na makongamano yote tutayafuta
-Sheria ya manunuzi nayo ni mdudu mbaya. kalamu ya 1000 hununuliwa kwa sh.10,000. Sheria hii lazima tuibadilishe
-Magari ya gharama kwa viongozi waandamizi wa serikali yatadhibitiwa

****Vipaumbele Vya Serikali Yangu
1.Kupunguza urasmu
2.Kubana matumizi
3.Kurejesha nidham ya serikali na utumishi wa serikali
4.Kupunguza ukubwa wa baraza la serikali
5.Tutaongeza nidhamu ya matumizi serikalini

==> Rais Magufuli amehitimisha Hotuba yake na kutangaza kulizindua Rasmi Bunge la 11


Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameahirisha bunge hadi tarehe 26 January mwaka 2015

Spika wa bunge Job Ndugai amesema bunge limesikitishwa na kitendo cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na wabunge wa upinzani na kuahidi kutotokea tena kwa kitendo kama hicho.

Bunge limeahirishwa...hadi mwezi Januari mwaka ujao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527