Picha..!!BAADA YA KUFANYA KWELI MONDULI...LOWASSA AWEKA HISTORIA NYINGINE PEMBA



Mgombea urais wa jamhuri ya mungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyo unda umoja wa katiba ya waanchi UKAWa Mh.Edward Ngoyayi Lowassa amewataka wananchi kisiwani pemba kumkataa na kuto mchagua mgombea yeyote anae chezea amani ya nchi kwani nchii hii similiki ya mtu bali nimali ya watanzania wote na kusisitiza kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anapambana na umasikini kwa nyanja zote.


Mh.Lowassa alie wasili kisiwani Pemba na kusindikizwa na vijana kwa Pikipiki Vespa na Magari hadi hapa kiwanja cha Kibirinzi ambapo mkutano wa kampeni ulifanyika na kuwataka wananchi wa Pemba kumkataa mgombea anae tishia amani na utulivu kwani ndio itakayo weza kusaidia kufikisha malengo ya kuleta mageuzi ya kweli katika nyanja zote za maendeleo na kuahidi kuwa ataimarisha Hospitali kila wilaya kwakuweka vifaa vya kisasa.

Mh .LowasSa amesisitiza kuwa endapo atakuwa rais wa Tanzania atahakikisha anabadilisha mitaala ya elimu kuwa ya kisasa ilikuliletea maendeleo ya haraka taifa la Tanzania.

Mapema mgombea mwenza wa rais wa jamhuri ya mungano wa Tanzania kupitia umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh.Juma Duni Haji amewataka wazanzibar kushirikiana ilikufanya mabadiliko kwa amani na utulivu nae mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF Malim Seif Sharifu hamadi ameendelea kussisitiza kuwa chama chake cha wananchi CUF hakina mpango wa kufanya vurugu kama inavyo daiwa.

Angalia picha hapa chini


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi, wakati akiwa njiani kuelekea kwenye Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Tibirinzi, Kisiwani Pemba leo Oktoba 3, 2015..





Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa akifurahi jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, walipokutana katika katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Tibirinzi, Kisiwani Pemba leo Oktoba
 3, 2015. .


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa akiwa ameusimamisha msafara wake kupisha watu wa huduma ya kwanza walikuwa wamembeba mama mmoja (jina lake halikupatikana kwa haraka) aliekuwa amepoteza fahamu kutokana na kukosa hewa katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Tibirinzi, Kisiwani Pemba leo October 3, 2015..











Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527