MIILI YA WANAJESHI WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA GARI HUKO KIGOMA YAAGWA



Mkuu wa jeshi la kujenga taifa,meja jenerali Raphael Muhuga ameongoza kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu askari wawili pamoja na vijana watatu waliokuwa wanapatiwa mafunzo ya JKT kambi la Bulombora JKT waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Kigoma.


Taratibu za kuaga miili hiyo kwa heshima zote za kijeshi zimefanyika leo mchana katika uwanja wa ndege wa kijeshi jijini Dar es Salaam na baadaye miili hiyo kusafirishwa kwa mazishi katika mikoa ya Mtwara, Pwani,Tanga, na jijini Dar es Salaam.

Majina ya askari hao wa kikosi cha Bulombora JKT waliofariki dunia katika ajali hiyo iliyotokea tarehe 01 oktoba 2015 majira ya saa 10 jioni ni Sajini Amidu,Ally Kambanga na Private Abel,Thadei Maisha.

Wengine ni vijana waliokuwa wanahudhuria mafunzo ya jeshi la kujenga taifa kwa kujitolea ambao ni Serviceman Said Sadala Said na Serviceman Eugen Stephano Butati waliokuwa katika mafunzo operasheni miaka 50 ya muungano.

Aidha wapo pia Recruti Abubakari Salum Washokera,Recruti Bakari Ramadhani Kibaya na Recruti Fredrick Kahemela Emphraim waliokuwa katika mafunzo operasheni Kikwete.

Makao makuu ya jeshi la kujenga taifa kwa kushirikiana na makao makuu ya jeshi la ulinzi la wananchi wa tanzania wameshaandaa ndege kubwa ya kijeshi itakayosafirisha miili ya marehemu hao kuletwa dar es salaam.

Aidha katika ajali hiyo askari wengine 23 wamejeruhiwa,kati yao wawili watahamishiwa hospitali kuu ya kijeshi Lugalo kwa matibabu zaidi.

Askari hao walikuwa kwenye gari la jeshi aina ya iveco 5717 jw09 ambapo walipata ajali maeneo ya mlima wa pasua umbali wa kilomita 11 kutoka Kigoma mjini,walikuwa wanakwenda kubadilishana zamu ya ulinzi katika moja ya kiteule cha ulinzi kilichopo mkoani Kigoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527