Maajabu!! KUTANA NA MTOTO ALIYEZALIWA BILA SEHEMU KUBWA YA FUVU LA KICHWA,SASA ATIMIZA MWAKA MMOJA





Jaxon Buell alizaliwa August 27, 2014 huko Birmingham, Uingereza akiwa hana sehemu kubwa ya fuvu la kichwa pamoja na ubongo. 

 
Brandon na Brittany ambao ni wazazi wake waliambiwa na madaktari kuwa ni vyema wakakubali kuitoa mimba ya mtoto huyo lakini hawakuwa tayari na hata mtoto huyo alipozaliwa waliambiwa hataweza kuishi muda mrefu kutokana na ukubwa wa tatizo lake.



Baada ya miezi mingi kupita akiwa anafanyiwa uchunguzi na madaktari waligundua kuwa hakuna kinga yoyote itakayomsaidia kuendelea kuishi lakini wazazi wake hawakukata tamaa na walifanya kila jitihada kuhakikisha mtoto wao anaendelea kuishi.


Wazazi wa Jaxon, Brandon na Brittany pamoja na mtoto wao wakiwa na nyuso za furaha


Wazi hao waliweza kukusanya kiasi cha dola 100,000 kutoka kwa watu mbalimbali ili kuokoa maisha ya mtoto wao tangu azaliwe na sasa ana miezi 13 na anaendelea vizuri.



Unaweza kuitazama na hii video yake hapa pia…

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527