GARI LA JESHI LASHINDWA KUPANDA MLIMA NA KUUA VIJANA SITA WA JKT BULOMBORA, KIGOMA

VIJANA sita waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi ya kujitolea katika kikosi cha 821 JKT Bulombora mkoani Kigoma wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya gari iliyotokea jana jioni

Mganga Mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Kigoma Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

"Ni kweli jana majira ya saa moja jioni tumepokea miili minne ya vijana wa JKT ambao waliletwa hapa tayari wamefariki na majeruhi 21.

 "Wengine wawili wamefariki hapa hapa wakati tukiendelea kuwapa huduma" alisema Dkt Fadhili.

Alisema hali za majeruhi mpaka sasa siyo nzuri sana kwani wengi wameumia sehemu za kichwa na mwilini.

"Bado tunaendelea na jitahada za kuwapatia matibabu na majina ya waliopoteza maisha pamoja majeruhi tutatoa kesho, sababu majeruhi wengi hawana fahamu"alisema.

Naye kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Afande Ferdinand Mtui alisema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo la jeshi kushindwa kupanda mlima na kusababisha tairi mbili za nyuma kupasuka.

Alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kasaka karibu na mizani ambapo lori hilo la jeshi lilikuwa likitoka mjini kwenda kambini likiwa limebeba makreti ya soda na unga.


Chanzo-Udakuspecially blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527