NIMEKUSOGEZEA PICHA 22 ZA MKUTANO WA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI LEO


Hapa ni katika kijiji cha Nhelegani Mashariki katika kata ya Kizumbi katika jimbo la Shinyanga mjini mkoani Shinyanga ambapo mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi mheshimiwa Stephen Masele ameendelea na mchakamchaka wa kampeni zake akitetea nafasi hiyo ya ubunge kwa awamu nyingine.Pamoja na kumwombea kura mgombea udiwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya,hakusahau kujipigia debe ili wananchi wamchague kuwa mbunge huku akiwaomba wakazi wa Shinyanga kumpa kura mgombea urais kupitia CCM Dkt John Pombe Magufuli.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde ametusogezea picha 22 kutoka eneo la mkutano angalia hapa chini


Awali mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini kanali mstaafu Tajiri Maulid akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kupuuza propaganda zinazoenezwa na viongozi wa Ukawa kuhusu kuibiwa kura ambazo alisisitiza kuwa Ukawa hawana kura za kutosha kuwawezesha ikulu hivyo hawana kura za kutosha kuibiwa


Meza kuu wakifurahia jambo eneo la mkutano...Mwenyekiti wa huyo wa CCM Tajiri Maulid aliwataka pia wananchi kupuuza kauli zinazotolewa na mgombea urais wa Ukawa mheshimiwa Edward Lowassa kuwa maji ya ziwa Victoria mkoani Shinyanga ameyaleta yeye na kuongeza kuwa maji hayo yameletwa na serikali ya CCM


Burudani nayo ilikuwepo pichani ni kikundi cha vijana wanaojiita Yamoto Band ya Shinyanga wakifanya yao jukwaani


Meza kuu wakicheza nyimbo za CCM


Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele akiwahutubia wakazi wa Kizumbi leo ambapo pamoja na kuwakumbusha wananchi mambo mbalimbali ya kimaendeleo aliyowafanya katika kipindi cha miaka mitani ya ubunge katika sekta mbalimbali kama vile afya,elimu,viwanda,barabara n.k aliwaomba wananchi wampe kura ili kuendelea kufanya mambo makubwa zaidi ya kimaendeleo katika jamii


Mkazi wa Nhelegani Mashariki katika kata ya Kizumbi akifuatiliwa kwa umakini zaidi kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano na fimbo yake yenye alama ya V


Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea


Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka vijana kupima hoja za wagombea badala ya kushabikia siasa zisizokuwa na tija za wapinzani wanaoendekeza siasa za majitaka za kuchafuana majukwaani


Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele aliwataka wakazi wa Shinyanga kuchagua viongozi wazawa badala ya watu wa kuja kama mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia Chadema/Ukawa Patrobas Katambi aliyedai siyo mkazi wa Shinyanga anatoka Sengerema mkoani Mwanza na ameletwa na Chadema Makao makuu kitendo ambapo alisema kimeivuruga Chadema jimbo la Shinyanga kwa kuletewa mtu wasiyemtaka


Mkazi wa Kizumbi akifuatilia kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano..mzee aliamua kusimama nyumba kabisa kutoka eneo la mkutano lakini kamera zetu zikamuona


Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano


Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele akimwombea kura mgombea udiwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya


Tunafuatilia kinachojiri hapa.....


Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele akizungumzia namna atakavyoshirikiana na mgombea udiwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya katika kuwaletea maendeleo wakazi wa Kizumbi wanaokabiliwa na changamoto ya migogoro ya ardhi/viwanja


Mkutano unaendelea


Kampeni meneja mkuu katika kata ya Kizumbi ndugu Mwakaluba Wilson Jacob akizungumza kwenye mkutano ambapo aliwataka vijana kuwa makini kwa kuchambua kwa kina kiongozi gani atawaondoa watanzania katika wimbi la Umaskini na kuongeza kuwa mtu sahihi ni Magufuli pekee badala la Lowassa fisadi


Wananchi wakiwa eneo la tukio


Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano


Baada ya mkutano kumalizika burudani ikaendelea..mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele na mgombea udiwani kata ya Kizumbi Reuben Kitinya wakicheza na kundi la Yamoto Band ya Shinyanga







Tunafuatilia kinachoendelea....


Mkutano umemalizika....


Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527