ASKOFU GWAJIMA-AMEJIBU HAYA KUHUSU DR SLAA...ASISITIZA KILICHOMTOA SLAA CHADEMA SIYO UFISADI WA LOWASSA...KUNA VIDEO PIA




Siku chache baada ya aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaakutangaza kwamba ameamua kuachana na Siasa, baada ya siku kadhaa kutoonekana kwenye Mikutano pamoja na Viko vya CHADEMA pamoja na Vyama vya UKAWA, stori ambazo zinamtaja yeye bado hazijaacha kuibuka.



Kulikuwa na madai ambayo yaliripotiwa na Vyombo vya Habari pamoja na kuandikwa sana Magazetini na Mitandaoni pia ambapo Maaskofu walitajwa kuhusishwa na Rushwa… Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima kaongea Dar es Salaam na waandishi wa habari jijini Dar es salaam… Kuna hizi baadhi ya sentensi alizosema.

Gwajima:'Lengo ni kufafanua maneno yaliyosemwa na rafiki yangu Dk.Wilbrod Slaa na kurushwa karibu kwenye TV zote....Kati ya maneno yaliyonigusa ni kusema "Gwajima aliniambia Maaskofu walipewa Rushwa ili kumsapoti Lowassa"

Gwajima: "Mara nyingi ananitaja mimi kuwa ni rafiki yake, siwezi kumkana kwa kuwa amekosea, ni rafiki aliyekosea...Urafiki wangu na Dk. SLAA ulianza akiwa CHADEMA katika harakati za Ukombozi kuitoa nchi katika matatizo"

Gwajima : Alipata matishio mengi ya kuuawa na kukamatwa, akaomba nimsaidie kumpa watu salama wa kumsaidia,Nilimpa Walinzi wanne wa kumlinda, aliogopa kulindwa na Polisi au watu wengine angesalitiwa.....Nilimpa Walinzi waaminifu waliokuwa wananilinda mimi, wamemlinda kwa zaidi ya miaka minne'

Gwajima:Nilimpa na mtu mwingine, mama mtu mzima wa miaka 50 akawa anampikia chakula nyumbani kwake'-

Gwajima: Nitakayoongea kuhusu Dk. SLAA nayajua kuanzia jikoni, chumbani na ni ya uhakika kabisa.

Gwajima :Dk. SLAA alisema amehama CHADEMA kwa sababu ya ujio wa LOWASSA, sio kweli....Ujio wa LOWASSA ulianza na Dr. SLAA mwenyewe, alikuja kuniomba nimsaidie wampate LOWASSA ili washinde Uchaguzi...…akasema mheshimiwa Lowassa ni mtu mwenye nguvu tukimpata yule tutashinda....

Gwajima: Mimi siko Kamati Kuu CHADEMA lakini niliomba niingie Kikao cha Kamati Kuu ili kuhakikisha LOWASSA amefika salama....Tulimaliza Kikao na SLAA saa sita usiku, baadaye nikaambiwa na Walinzi kuwa mke wa SLAA alimfungia nje.

'Nilienda kwa SLAA akaniambia ameamua kujitoa kwenye Siasa kwa sababu Familia yake inavunjika.

Gwajima:"Dr Slaa mwenye nguvu,ametekwa...kwanini mtu maarufu ana behave namna hii....,Josephine alikuwa amejipanga kuwa First lady..mimi ndiyo first lady".

Gwajima: Lowassa ni rafiki yangu..Slaa ni rafiki yangu...Lowassa alikuwa rafiki yangu alipokuwa  CCM...na Lowassa ni mtu anayekuja haraka akiitwa mahali...

Gwajima ameonyesha meseji aliyotumiwa na Dr. Slaa kuhusu kustaafu kwake siasa.Angalia Video hapo chini kabisa

Gwajima: Kama Dr. Slaa anakana aje atoke hapa akane aone mambo ya mshenga yalivyo, watu wanashangaa Slaa anaweza kufanya haya! Si yeye ni mama. Slaa alikuwa adili, sasa uzoefu wa ndoa hana, bora sisi wachungaji tunaoa.

Nilimpa maneno ya matumaini, nitamtafuta mkewe niongee nae, nilimtafuta mkewe Rose Garden. 

Nilianza mimi kumbembeleza amruhusu baba aendelee na hayo maelezo nimeyarokodi na mimi ni mtu wa kurekodi. 

Alisema ameshawaambia watu yeye atakuwa first lady, siku iliyofuata tarehe 28, nilimuita yule mama Kibo complex.

Tukakaa ndani ya gari yake, nilikuwa mimi na mtu mwingine, niliendelea kurekodi tena.

 Ilikuwa ni siku Lowassa anapokea kadi bahari beach, nawaonyesha hio sio kwa mumuone Slaa mbaya. 

Saa nane mchana akasema nimekubali Slaa arudi aingie kazini kwa sharti mkutano wa kumpokea Lowassa ufutwe. Nikamwambia hilo halitatokea milele.

Watu wengi sana wametumwa kuongea na yule mama, akiwemo mzee Ndesamburo ambae alishindwa kumpata yule mama, kumbe yule mama anaongea kwa karibu sana na mchungaji Max hivyo akampeleka Ndesa.

Mchungaji Max: Ilifika mahali chama kiliacha majukumu yote kumpata yule mama kuongea na Ndesamburo, yule mama alisema CHADEMA wanacheza mpaka waongee nami, alisema CHADEMA ni waongo na wanafiki, kwanini watufanya mpaka tumekosa urais. 

Mpaka juzi nilikuwa nawasiliane nae lakini maongezi yake kwa ujumla anasema kwanini wameachwa kugombea Urais, kwa jinsi alivyokuwa anaongea nikajua hata Dokta hawezi kuchomoka.

Slaa alisema Josephine amemfungia Serena, ukweli mimi naufahamu, ishu ipo kwa mkewe, Dr tumeshampoteza.

Gwajima: Siku moja nilikuwa Korea, Slaa alisema mkewe amedondoka amezimia, nikaomba kwenye simu mkewe akaanza kupiga kelele, nilimwambia Dr. Slaa sijawahi kuona mambo haya. 

Nilikuwa namsindikiza mke wangu kwenda London, cha kushangaza nikamkuta mke wa Dr Slaa airpot amekuja kusindikiza, umeambiwa na nani! Akasema nimejisikia tu! Baada ya check in, kurudi mke wa Dr. Slaa alidondoka chini, mashetani yalikuwa yanamrudia.

Siku nyingine Slaa alinipigia simu mkewe amedondoka, haya ni mashetani, Slaa anaongozwa na mwanamke wa aina hii. Ikulu pangekalika? Slaa si yeye, kuna tatizo limetokea.

Slaa Serena alisema kwenye mkutano wa CHADEMA watu waliletwa na malori na mabasi, mlioenda mjiulize ni kweli? Mtu anaesema uongo wa mchana, anasema Gwajima anasema maaskofu wa katoliki wamepewa hela. Kanisa katoliki ndio kanisa credible sana duniani.

Kwanini Slaa amesema! Kwanza kuwaondolea credibility, maaskofu hawa wamemsomesha, leo maaskofu 30 anawasingizia. Kwa mtu unaemuamini Slaa unaweza kusema anasema kweli lakini nimekuonyesha mazingira kwanini!

Anatukana maaskofu wa protestant na katoliki, nani aliemtuma! Slaa aliulizwa unalindwa na usalama wa taifa? Alisema kweli, watu wa usalama wanambeba kwenda Serena, Azam na Star Tv kutukana maaskofu. 

Maaskofu hawaruhusiwi kujihusisha na siasa lakini ni wapiga kura, Je, atakupa kura! Je waumini wao watakupa kura! Strategy hii imeshindikana wafikirie nyingine. Bahati mbaya hii ilikuwa silaha yao ya mwisho.

Mababa askofu wa kanisa katoliki hawakupewa rushwa wala mimi sijapewa rushwa, anasema nilikuwa nazunguka kwenye ndege na Lowassa. Mimi nina ndege yangu na siombi kibali kuzungumza mtu.

Usalama wa taifa sio wa CCM, mnatafasiriwa nyie ndio mnatukana maaskofu, usalama wa taifa mnamuharibia Magufuli, mwacheni aendelee kampeni zake kwa amani. 

Siku nitakayorudi kumjibu Slaa akinisemesha, nitasema Slaa alivyokutana na watu wa usalama wa taifa Afrika kusini. Usalama mtapomuongoza tena huyo mtu wenu wenu atukane maaskofu, nitawalipua na bomu na macho yenu hamtafungua tena
Uadilifu wa Slaa

Gwajima: Alisema baba askofu lazima mtubu, najiuliza yeye ni msafi kuliko sisi? Slaa aliacha wito ambalo ni tatizo tayari, zaidi ya kuacha wito ukaoa! Nikija tena nitaleta watoto aliowazaa na uhusiano wa yeye kutoka. Ukaa na mke na watoto ukatelekeza, haitoshi ukaenda kuoa mke wa mtu mwingine. Kamili akaweka zuio mahakamani.

Slaa alisema Ridhwani nauza madawa ya kulevya, leo Slaa ndio anao aliowasema, anaemuongoza Slaa akome na akome kabisa. Watu wa usalama kazi yenu ni kulinda nchi iwe na amani na sio kuichafua.


Kinachosumbua ni wakati na majira, 20 kabla ya kristo kulikuwa ana mtu aliehubiri ubudha, akaijaza Ubudha kwa sababu yalikuwa majira yake. Baada ya hapo, karne ya kwanza alitokea Yesu kristo na kukutana na upinzani wa ajabu, ukifika wakati waksema wamemkamata. 

Kweli ukiizika ina tabia ya kufufuka na ukiizika haiwezi kufa tena, akaja kutokea Mtume Muhammad japo alipata upinzani mkubwa leo Uislam umeenea sana. Nami niseme mfate majira, msishindane nayo. Tanzania ni kubwa kuliko watanzania.
SIKILIZA HAPA ASKOFU GWAJIMA AKIELEZA NAMNA ALIVYOMFAHAMU DR SLAA



Angalia hapa chini Gwajima akionyesha Ushahidi wa SMS aliyotumiwa na Dr Slaa baada ya Kufungiwa nje na mke wake  


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527