Vurugu Bungeni Dodoma!! BAADA YA WATANO..WABUNGE WENGINE ZAIDI YA 30 WAPIGWA "STOP" KUINGIA BUNGENI TANZANIA KWA MUDA WA SIKU 5



Kumekuwa na story mfululizo toka ndani ya Kikao cha Bunge, Dodoma kwamuda wa siku tatu mfululizo zimetokea vurugu, Kikao kimeahirishwa kwa siku mbili mfululizo.

Alhamisi July 02 2015 Mbunge John Mnyika aliomba mwongozo kuomba Bunge lisiendelee kwa vile ishu ya kujadili Miswada mitatu kwa siku moja ilikuwa inakiuka Kanuni za Bunge, ukatokea mvutano na baadae Spika AnneMakinda akaahirisha Bunge.

Ijumaa July 03 2015 hali ikawa hivyohivyo tena, wakati Waziri George Simbachawene anasoma Muswada, ikatokea mvutano mwingine, zikaanzishwa kelele Bunge likaahirisha tena.. Kikao cha Jioni Spika Anne Makinda akarudi na list ya majina ya Wabunge ambao wamesimamishwa Bungeni kutokana na maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Bunge.

Leo July 04 2015 Kikao kimeanza tena saa tatu asubuhi, Mbunge Ezekiel Wenje akaomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?

Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… Spika akataja list ya Wabunge wengine ambao wanasimamishwa kuhudhuria Vikao vya Bunge kwasiku tano kila mmoja.

Ezekiel Wenje

Mussa Kombo

Masoud Abdallah Salim

Rebecca Ngodo

Sabrina Sungura

Khatib Said Haji

Dr. Anthony Mbassa

Maulidah Anna Valerian Komu

Kulikoyela Kahigi

Cecilia Pareso

Joyce Mukya

Mariam Msabaha

Grace Kiwelu

Israel Natse

Mustapha Akonaay

Konchesta Rwamlaza

Suleiman Bungura

Rashid Ali Abdallah

Ali Hamad

Riziki Juma

Rukia Kassim Ahmed

Azza Hamad

Khatibu Said Haji

Kombo Khamis Kombo

Ali Khamis Seif

Haroub Mohammed Shamisi
Kuruthum Jumanne

Mchuchuli

Amina Mwidau

Mkiwa Kimwanga

Salum Baruhani

Marry Stellah Malaki

Rashid Ally Omary

Mwanamrisho Abama

Lucy Owenya



Nje ya ukumbi wa bunge wabunge hao waliotolewa nje wakazungumza na waandishi wa habari wakaelezea kitendo cha wao kutolewa nje pamoja na sababu za wao kuikataa miswada hiyo kuletwa yote pamoja na kwa hati ya dharura.


 
Hata hivyo baada ya vurugu zote kuisha miswada yote mitatu ambayo ni sheria ya petroli, sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi pamoja na sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ambapo akiwasilisha muswada wa petroli bungeni mjini dodoma waziri wa nishati na madini Mh.Simba Chawene amesema mswada huo utajenga mfumo imara wa kusimamia sekta ya mafuta na gesi.
 



Wenyeviti wa kamati hizo nao wakawasilisha maoni na ushauri wa kamati zao ambapo mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini Mh. Richard Ndassa akisoma mani ya kamati amesema kamati imekubalina na serikali kuhusu mamlaka aliyopewa waziri pamoja na maoni ya wadau kuhusu kumuongezea waziri mamlaka kisheria kuingia mikataba mikubwa ya miradi ya gesi asilia pasipo kuingilia au kuwa na mamlaka sawa na TPDC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527