EDWARD LOWASSA AFUNGUKA MAZITO_KUHUSU AFYA YAKE,CHUKI,KUHAMA CCM,ELIMU,AJIRA........KUWASHA MOTO ARUSHA!

lowassa2

Moja ya story kubwa kwenye siasa za Tanzania wiki iliyopita ilikuwa ishu ya CCM kuwafungulia makada wake sita ambao walikiuka kanuni za chama hicho kwa kutangaza kugombea Urais mapema kinyume na utaratibu wa chama hicho, mmoja ya waliokuwa wamefungiwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.


Jana kulikuwa na stori ya Naibu Waziri Mwigulu Nchemba kutangaza kugombea Urais wa Tanzania kupitia CCM.. leo Mbunge Edward Lowassa ameongea kuhusu mambo kadhaa ikiwemo hali ya afya yake, chuki kwenye siasa, na ujumbe wake kwa CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Tanzania.
Waziri Mkuu mstaafu  Edward Lowassa leo amefanya  mkutano maalum nyumbani kwake mjini Dodoma  na  wahariri  wakuu  wa  vyombo  mbalimbali  vya  habari  hapa  nchini.Katika mkutano huo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter Serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo . Katika mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema yafuatayo;

1. Amesema Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji.

 Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya Mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta.

Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii.(Jumamosi)

2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono.
3. Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo kwanza .Amesema serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo na kuweka kando elimu. Ametangaza kuwa sera yake ni Elimu Kwanza."Tukiwekeza vizuri katika elimu tunaweza kubadilisha nchi yetu.. Tukitaka kuokoa nchi yetu tuwekeze kwenye elimu"-Lowassa.

4. Kuhusu pesa anasema anapata michango ya rafiki zake na ataendelea kupokea michango hii wakati wote wa harakati zake na haina madhara yotote.

5. Anasema hatahama CCM na asiyemtaka yeye CCM ndiye aondoke ndani ya chama kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi kuwania urais.
"Kuhama chama sina mpango.. nimeingia CCM toka 1977 sijafanya kazi mahali pengine popote isipokuwa CCM.. My life is CCM.. huyo ambae hanitaki CCM ndio ahame sio mimi nihame" Edward Lowassa.
 
6. Amesema hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa. Amemwachia Mungu kwani yeye ni mcha Mungu. 
“Mimi ni Mkristo, ninaamini kwenye dini yangu sana… sina kisasi na mtu yoyote“>>>Lowassa
7."Kuna chuki imeibuka kwenye siasa za nchi yetu na kutakiana mabaya, afya ni neema kutoka kwa Mungu.. mimi niko sawa kabisa kwa chochote kile.. kwenye Chama chetu waweke utaratibu tukapimwe wote afya mimi nitakuwa wa kwanza kwenda kupima tuelezane nani mgonjwa"-Lowassa.
8. Amesema Arusha itawaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio kwani ataanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi ijayo.

9.Sentensi yake nyingine kuhusu tatizo la ajira>>>”Tatizo la ajira ni bomu lisiposhughulikiwa.. toka nimetoka Serikalini kuna vitu ambavyo kama tungevifanya kwa kasi ile ambayo tulianza nayo ningepita napunga mkono nikapata kura zote, hatufanyi maamuzi iwe magumu au rahisi.. mambo yanakwenda legelege, Rais amefanya jitihada kubwa sana lakini kuna mambo hayaendi>>> Edward Lowassa.



10.“Upinzani umeanza kupata nguvu kubwa sisi ni chama dola tusibweteke.. wenzetu wanajiandaa vizuri na sisi tujiandae vizuri. Tusifanye mchezo tusibweteke”>>> Mbunge Edward Lowassa.


Kwa dakika tatu kayazungumza haya, sauti yake unaweza kuisikiliza hapa kwa kubonyeza play !!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527