Kali ya Shinyanga Leo!! MWENYEKITI WA MTAA APIGWA,AVUNJWA MGUU KWA TOFALI KISA KUKOJOA KWENYE UKUTA WA MTU!!




Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwenyekiti wa mtaa wa Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga Jumanne Maziku amevunjika mguu wa kushoto baada ya kupigwa tofali baada ya kukutwa akijisaidia haja ndogo kwenye ukuta wa nyumba ya mtu iliyopo karibu na baa.

Tukio hilo limetokea usiku wa kumkia leo katika eneo la Ngokolo Mitumbani  mjini Shinyanga baada ya mwenyekiti huyo kudaiwa kujisaidia kwenye ukuta wa nyumba ya mwanamke mmoja mkazi wa Ngokolo. 

Akizungumza na Malunde1 blog akiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyanga akisubiri rufaa ya kwenda hospitali ya Bugando jijini Mwanza mwenyekiti huyo amesema haya:>>

“Ilikuwa majira ya saa mbili,nikiwa na wenzangu tukinywa pombe,ghafla nikapigiwa simu na mtu nikainuka,hapo kuna mti na mazingira ya vichaka vichaka,nikaanza kuzungumza na simu baadaye nikaanza kujisaidia”>Jumanne Maziku.


Wakati naendelea kujisaidia,akaja jamaa mmoja akaniuliza,kwanini unajisaidia hapa?,mimi sikumsemesha,nikaanza kurudi kwa wenzangu pale kwenye grocery ghafla nikaanza kupigwa,huenda aliyenipiga ni kijana wake na mama mwenye nyumba,sasa hivi ndiyo anasimamia matibabu yangu”>Maziku

Maziku  amesema kitendo alichofanyiwa ni udhalilishaji kwake kwa sababu hakuwa najisaidia katika nyumba hiyo.

Naye mama mwenye nyumba alikokutwa anakojoa amesema ameambiwa atoe shilingi laki 7 kwa ajili ya matibabu ya mwenyekiti huyo wa mtaa aliyepigwa tofali.

Hata hivyo wa bar alikokuwa anakunywa pombe bi Halima Kisena amesema kitendo cha mwenyekiti wa mtaa kupigwa tofali kinatokana na ulevi wake na si kukosekana kwa vyoo katika baa zake.

“Katika bar zangu zote kuna vyoo,sijui kilichompeleka huko na kujisaidia kwenye ukuta wa watu,ulevi wake ndiyo umemponza”,amesema Kisena.

Na Mwandishi maalum wa Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527