Inatisha !! JOTO LAPANDA KWA KASI YA AJABU,LAUA WATU 430 HADI SASA,MAGARI YASIYO NA VIYOYOZI HALI TETE!!

 

Takriban watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.

Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzi joto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
 
Vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.

Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzi joto 48C huku wakazi wa mji mkuu wa India New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzi joto 44C .

Maafisa wa utawala nchini humo wameanza kampeni ya kuwahamasisha wananchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanywe waji mengi.

Yamkini viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.

Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246 waliopoteza maisha yao kuanzia juma lililopita.

"asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema kamishna wa kupambana na majanga katika jimbo la Andhra Pradesh.

Waaandishi wa habari wanasema kuwa watu 186 wameaga dunia katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.

Watu 58 wamekufa kuanzia siku ya Jumamosi.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadhaa zijazo.

Watu wengine kumi walipoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.

Waendesha teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano katika mji mkuu wa Kolkata. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527