WAKILI MKENYA ATANGAZA KUMUOA MTOTO WA OBAMA,ANGALIA HAPA MIKAKATI YAKE!! MAHARI NG'OMBE 50,KONDOO 7O NA MBUZI 30!

Obama-Funny-Face

Kila mtu ana ndoto na mtu ambaye anamhitaji awe mpenzi wake kwa maisha yote, sio ajabu mtu akawa na ndoto za kumuwaza mtu ambaye ni ngumu sana kwenye mazingira ya kawaida kuonana nae, pata picha ya huyu jamaa ambaye yeye macho na akili yake ni kwa Malia Obama.

Kiprono Matagei kazi yake ni wakili Kenya, ndoto yake ni yeye na Malia Obama damdam, alianza kumpenda tangu mwaka 2008.. moyoni mwake akaweka ahadi kwamba hatokuwa na uhusiano na mwanamke yoyote mpaka siku ampate Malia wake !!

Jamaa kajiongeza kabisa, amesema mahari aliyopanga kutoa ni hii>>> ng’ombe 50, kondoo 70 na mbuzi 30.
wakili
Kiprono kasema yuko serious kabisa na aliwashirikisha familia yake, wako tayari nao kumsaidia mpaka afanikiwe !!
** FOR USE AS DESIRED WITH YEAR END--FILE **In this July 4, 2008 file photo, Democratic presidential candidate, Sen. Barack Obama, second from right, and his wife Michelle, left, watch an Independence Day parade with their two daughters, Malia, right, and Sasha in Butte, Mont. (AP Photo/Jae C. Hong/FILE)
Obama atakuwa Kenya mwezi wa saba, ziara yake haitachukua muda mrefu lakini jamaa amesema atajitahidi aitumie nafasi hiyo hiyo kumuona ‘baba mkwe huyo mtarajiwa’ !!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527