BASI LA UNIQUE EXPRESS LAGONGANA NA LORI LA COCACOLA SAMUYE SHINYANGA,WATU 10 WAFARIKI,MAJERUHI 50

Miili ya abiria ikiwa imenasa katika basi la Unique

Ajali za barabarani zimeendelea kujitokeza ambapo leo majira ya saa tisa kasorobo alasiri Watu 10 wamefariki dunia na wengine 50 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Unique Express lenye namba za usajili T148 BKK kugongana na lori aina ya scania lenye namba za usajili T207 BSA na tela lenye namba za usajili T635 AJT mali ya kampuni ya Coca Cola katika barabara ya Tinde Shinyanga eneo la kijiji cha Ibingo kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Mashuhuda wa tukio wameiambia Malunde1 blog kuwa dereva wa lori alikuwa anaendesha gari akiwa katikati ya barabara huku dereva wa basi akiwa katika mwendo kasi hali ambayo katika kukwepa basi hilo aligonga tela la lori kisha kupinduka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha aliyeko eneo la tukio amesema watu 10 wamepoteza maisha katika ajali hiyo kati yao 9 walifariki dunia papo hapo huku majeruhi 50  wakiwemo wanawake 13,wanaume 36 na mtoto mmoja  wa kiume wanapata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527