|
Wafuasi wa Lowassa wakiwa na watoto katika kituo cha Buhangija
|
|
Marafiki wa Lowassa wakiwa getini wakitafakari jambo kabla ya kuingia ndani-
Leo kikundi cha Vijana mkoani Shinyanga wanaouunga mkono
harakati za waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ikiwemo kuchukua fomu ya kugombea urais wametembelea
kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino)cha Buhangija Jumuishi katika manispaa ya Shinyanga na kushiriki shughuli za ujenzi wa jengo la huduma za afya linalojengwa na Wahindi ,kufanya usafi na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa ajili ya watoto 390 waliopo katika kituo hicho-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
|
|
Bango kubwa lililokuwa limebebwa na marafiki wa Lowassa( Friends of Edward Lowassa 4U Movement) wakiamini katika Umoja,Utumishi,Uwajibikaji na Uzalendo |
|
Baada ya kuingia Kituoni-Marafiki
wa Lowassa wakishiriki shughuli za ujenzi wa jengo la afya linalojengwa na
Wahindi/wananchi |
|
Marafiki wa Lowassa kupitia 4U Movement wakishiriki shughuli za ujezi,hapa wanachanganya zege |
|
Wanaendelea na ujenzi |
|
Wanachanganya zege |
|
Kulia ni Afisa
habari wa marafiki wa Lowassa mkoa wa Shinyanga Musa Jonas akishiriki shughuli
ya ujenzi katika kituo cha walemavu cha Buhangija |
|
Marafikiwa
Lowassa mkoa wa Shinyanga wakifua nguo za watoto wanaolelewa katika kituo cha
Buhangija Jumuishi mjini Shinyanga |
|
Wafuasi/marafiki wa Lowassa wakifua nguo za watoto hao
|
|
Marafiki wa Lowassa wakifagia na kuchoma moto taka |
|
Hawa wanaanika nguo baada ya kumaliza kufua |
|
Zoezi la kufua nguo linaendelea |
|
Miongoni
mwa mabango yalikuwa yamebebwa na marafiki wa Lowassa |
|
Marafiki wa Lowassa wakiwa wamebeba mabango |
|
Mabango yalikuwa mengi |
|
Mabango yakachukua nafasi zaidi |
|
Wafuasi wa Lowassa wakiwa na watoto katika kituo cha Buhangija |
|
Watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasiosikia na wasioona |
|
Kushoto ni Mwenyekiti/mratibu
wa 4U Movement wilaya ya Shinyanga Ramadhan akizungumza katika kituo cha
walemavu wa ngozi Buhangija mkoani Shinyanga |
|
Mwenyekiti ambaye ni mratibu wa marafiki wa Lowassa mkoa wa
Shinyanga Hassan Haruna akizungumza katika kituo hicho ambapo alisema wameamua kufika katika kituo hicho ili kuunga
mkono jitihada zinazofanywa na serikali kupiga vita mauaji ya albino nchini na kuutangazia umma kwamba wanaamini
kabisa kuwa kiongozi atakayeweza kuwatetea albino ni Edward Lowassa,kwani
amefanya mambo mengi makubwa nchini,hivyo kitendo cha kukomesha mauaji haya
itakuwa kazi rahisi kwake,hivyo kumshawishi achukue fomu ya urais muda ukifika.
|
|
Marafiki wa Lowassa wakijiandaa kukabidhi msaada wa
maharage,unga,mkaa,sabuni,chumvi,maji,soda,mafuta
ya kujipaka na mafuta ya kupikia. |
|
Zoezi la kukabidhi msaada linaendelea,kulia ni mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali akipokea mfuko wa unga |
|
Kulia ni mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali akizungumza baada ya kupokea msaada kutoka kwa vijana hao
ambapo alisema hivi sasa kituo hicho kina watoto 390,kati yao wenye
albinism ni 286,wasioona 40 na wasiosikia 64,na kwamba changamoto kubwa zaidi
ni chakula kwani kwa mlo mmoja tu zinahitajika kilo 60 za unga,32 za maharage,70 mchele na nyama
kilo 33,hivyo chakula kinahitajika--Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
|
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527