Taarifa Rasmi na Picha_ AJALI YA BASI LA UNIQUE EXPRESS KUUA WATU 10 SHINYANGA




Watu 10 wamefariki dunia na wengine 50 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Unique Express lenye namba za usajili T148 BKKkugongana na lori aina ya scania lenye namba za usajili T207 BSA na tela lenye namba za usajili T635 AJT mali ya kampuni ya Coca Cola katika barabara ya Tinde Shinyanga eneo la kijiji cha Ibingo kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Habari Kamili iko chini ya picha zote

Maafisa wa polisi na wataalam wa afya kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la ajali.Mashuhuda wa tukio wameiambia Malunde1 blog kuwa dereva wa lori alikuwa anaendesha gari akiwa katikati ya barabara huku dereva wa basi akiwa katika mwendo kasi hali ambayo katika kukwepa basi hilo aligonga tela la lori kisha kupinduka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akiwa upande wa basi walikolaliwa abiria watatu kabla ya basi kuinuliwa kwa winchi
Wataalam wa afya wakiangalia miili iliyonasa kwenye basi
Basi likiwa limepinduka
Tela la lori la kampuni ya Coca cola lililokuwa linaelekea Shinyanga
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha aliyekuwa eneo la tukio amesema watu 10 wamepoteza maisha katika ajali hiyo kati yao 9 walifariki dunia papo hapo huku majeruhi 50  wakiwemo wanawake 13,wanaume 36 na mtoto mmoja  wa kiume wanapata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akitoa maelekezo kwa askari polisi na kikosi cha uokoaji na wataalam wa afya eneo la ajali
Miili ya marehemu ikiwa imenasa kwenye basi

Kulia ni Kelvin Moshi mkazi wa Tanga aliyenusurika ifo katika ajali hiyo,aliyekuwa anasafiri kutoka Mwanza kwenda Tabora amesema dereva wa basi alikuwa katika mwendo kasi hali ambayo ilimfanya basi limshinde na kugongana na lori hilo.

Miili ya marehemu ikiwekwa kwenye lori baada ya kutolewa kwenye basi

Basi la Unique Express baada ya kuinuliwa na kuondoa miili ya watu watatu waliokuwa wamenasa kwenye basi

Maafisa wa polisi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio,Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog.


Watu 10 wamefariki dunia na wengine 50 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Unique Express lenye namba za usajili T148BKK kugongana na lori aina ya scania lenye namba za usajili T207 BSA na tela lenye namba za usajili T635 AJT mali ya kampuni ya Coca Cola katika barabara ya Tinde Shinyanga eneo la kijiji cha Ibingo kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo imetokea Leo majira ya saa 9 kasorobo alasiri wakati basi hilo likitokea jijini Mwanza kuelekea mkoani Tabora.

Mashuhuda wa tukio wameiambia Malunde1 blog kuwa dereva wa lori alikuwa anaendesha gari akiwa katikati ya barabara huku dereva wa basi akiwa katika mwendo kasi hali ambapo katika kukwepa basi hilo aligonga tela la lori kisha kupinduka.

Mmoja wa walionusurika kifo katika ajali hiyo Kelvin Moshi mkazi wa Tanga aliyekuwa anasafiri kutoka Mwanza kwenda Tabora alisema dereva wa basi alikuwa katika mwendo kasi hali ambayo ilimfanya basi limshinde na kugongana na lori hilo.

“Dereva wetu alikuwa katika mwendo kasi,akalikwepa basi na kugonga tela la lori lililokuwa linapandisha mlima katika barabara na kupinduka mara kadhaa,ajali hii imetokana na uzembe wa dereva wetu”,alieleza  Moshi.

Diwani wa kata ya Samuye Amos Shija alisema dereva wa basi alikuwa katika mwendo kasi basi likamshinda kisha kugongana na basi hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha aliyekuwa eneo la tukio alisema watu 10 wamepoteza maisha katika ajali hiyo kati yao 9 walifariki dunia papo hapo huku majeruhi 50.

“Watu 10 wamefariki dunia,miili mitatu ya marehemu ilinasa kwenye gari,majeruhi  waliopo ni 50 wakiwemo wanawake 13,wanaume 36 na mtoto mmoja  wa kiume wanapata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga,wapo walio katika hali mbaya akiwemo dereva wa basi,tunashukuru wananchi wametusaidia kusaidia majeruhi na kuondoa miili ya watu walionasa kwenye basi”,alieleza Kamanda Kamugisha.

“Basi lilikuwa linatoka Mwanza kwenda Tabora,chanzo ni uzembe wa dereva na mwendo kasi wa basi wakati huo huo dereva wa lori alikuwa anaendesha gari akiwa katikati ya barabara,ndipo yakagongana na kusababisha vifo na majeruhi”,alieleza Kamanda Kamugisha.

Kamanda Kamugisha alisema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.


Alisema tayari dereva wa lori anashikiliwa na jeshi la polisi huku akiwataka madereva kuzingatia sheria za baarabarani ili kuepuka ajali zisizokuwa za lazima.
Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527