HAIJAWAHI KUTOKEA -ANGALIA PICHA TUKIO LA KIHISTORIA BLOGGERS ZAIDI YA 100 WA TANZANIA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM





Usiku wa Februari 28,2015 ni siku ambayo itakuwa siku ya historia ya kukumbukwa nchini Tanzania ambapo Bloggers zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani na waratibu wa mitandao mingine ya kijamii kama vile Forums wamekutana jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Makii uliopo Hotel ya Serena katika hafla ya Mwaka ya Kuwakutanisha Bloggers Tanzania kupitia Chama Chao maarufu “Tanzania Bloggers Network_TBN”-Picha zote kwa hisani ya Malunde1 blog

Picha za kumbukumbu wakati wa hafla hiyo-
Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga  huku malengo yake yakiwa ni kuwaunganisha bloggers,washika dau mbalimbali wa ulimwengu wa habari na mawasiliano(ikiwemo mitandao ya kijamii),kuzitambulisha na kuhakikisha kuwa blogs zinatambuliwa rasmi kama vyombo vya habari na vyanzo muhimu vya habari zenye kuelimisha,kufundisha,kuonya na kuburudisha.

Bloggers katika pozi-
Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga  huku malengo yake yakiwa ni kuwaunganisha bloggers,washika dau mbalimbali wa ulimwengu wa habari na mawasiliano(ikiwemo mitandao ya kijamii),kuzitambulisha na kuhakikisha kuwa blogs zinatambuliwa rasmi kama vyombo vya habari na vyanzo muhimu vya habari zenye kuelimisha,kufundisha,kuonya na kuburudisha.



Lengo jingine la mkutano huo ni kutilia mkazo fursa maalum iliyopo ya kuona blogs zinaleta mchango mhimu katika maendeleo ya kijamii,kisiasa na kiuchumi na pia amani na mshikamano nchini Tanzania.

Cheers!!
Mkutano huo pia ulikuwa unalenga kuunda mchakato mahsusi wa ushirikiano kati ya blogs a vyombo vingine vya habari kama vile magazeti,radio na televisheni pamoja na kukuza na kuendeleza dhana chanya ya uhuru wa fikra,mawazo na upatikanaji na upashanaji wa habari.
Lengo jingine ni kuhakikisha kwamba bloggers wote nchini Tanzania wanafuata na kuongozwa na misingi muhimu ya habari na mawasiliano kwa kupeana maarifa na miongozo mbalimbali kupitia semina,warsha na njia zinginezo za mafunzo.

Bloggers wakiendelea kupiga picha za pamoja,Kushoto ni ndugu Kadama Malunde,wa Malunde1 blog kutoka mkoani Shinyanga

Kushoto ni Othman Michuzi ambaye ni blogger maarufu na mkongwe nchini Tanzania


Wa kwanza kulia ni Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga  akisalimiana na Bloggers baada ya kuwasili ukumbini
 Kushoto ni mkurugenzi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga akiwa na baadhi ya viongozi wa Tanzania Bloggerr Network

Wadhamini wa hafla hiyo walikuwa Vodacom Tanzania,Benki ya NMB,Cocacola,AIM GROUP na kampuni ya huduma za intaneti ya Raha

 Bloggers wakibadilishana mawazo ukumbini-Mbali na mitandao mingine ya kijamii kama vile facebook,Twitter na Instagram,siku hizi Blogs zimekuwa chanzo kikubwa cha habari na mawasiliano na nchini Tanzania blogs zimekuwa mstari wa mbele zaidi katika kuwafikishia wananchi habari kwa haraka zaidi kwa Kiingereza wanasema "Breaking News"
Bloggers waliokutana ni zaidi ya 100,lakini Nchini Tanzania kuna Bloggers zaidi ya 500 na kinachofanyika sasa ni kukamilisha zoezi la kuwaunganisha bloggers wote ili kutambuana na kubadilishana maarifa na taarifa nyingi zaidi na kwa haraka zaidi
 
 Siku hizi taarifa nyingi zimekuwa zikianza kutoka kwenye blogs kisha baadae kusikika kwenye vyombo vingine vya habari na hapo ndipo umuhimu wa blogs unapoonekana kuwa na nguvu kuliko vyombo vingine vya habari ukiamchilia mbali radio
Bwana Rocky akiwa na Kadama Malunde ukumbini

 Bloggers wanateta neno
Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi akizungumza ukumbini ambapo alisema ni vyema sasa Blogs zikatambuliwa rasmi na mamlaka husika pamoja na taasisi zinazohusika na usimamizi wa tasnia ya habari likiwemo Baraza la Habari Tanzania(MCT),Idara ya Habari(Maelezo),MISA-Tan na hata mfuko wa ruzuku kwa vyombo vya habari nchini Tanzania(TMF)
Bloggers hao pia walilia kupewa Semina za MCT,kupewa vitambulisho(Press Card),kushiriki katika mafunzo na hata mashindano ya kila mwaka ya wanahabari yanayoandaliwa na MCT
 Kushoto ni Father Kidevu akionesha vituko vyake ukumbini


Msanii Jikoman akitoa burudani ukumbini

Risala ya TBN inasomwa kwa mgeni rasmi

Pozi ukumbini,kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya mapokezi katika hafla hiyo bwana Mkala Fundikira

 Bloggers wakiwa na mgeni rasmi ukumbini

Mgeni rasmi Kajubi Mukajanga alisema Baraza la Habari Tanzania linatambua na kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Bloggers wa Tanzania na kuahidi kuanzia mwaka huu kuwashirikisha katika fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo,tuzo kwa Bloggers na fursa zingine mbalimbali huku wakipanga mikakati ya kuwa na muongozo wa maadili kwa Bloggers wa Tanzania ili kuhakikisha kuwa habari wanazotoa zinakuwa na usawa,uhakika,ukweli  n.k


Mgeni rasmi,Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga akikata ndafu
Ndafu ukumbini

Mgeni rasmi ,Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga  akifungua burudani ya muziki

Ebwana eeee full burudani

Picha za kumbukumbu,kulia ni Rozy Ndauka ambaye ni msanii wa filamu nchini akiwa na Kadama Malunde wa Malunde1 blog

picha za kumbukumbu

Bloggerr katika pozi,kushoto ni Frdy wa Blogs za Mikoa

Bloggers katika pozi

Picha ya pamoja Bloggers

picha ya pamoja

picha ya kumbukumbu

Bloggers na mgeni rasmi
picha ya pamoja Bloggers na mgeni rasmi
Bloggers katika Wassira Style

picha ya kumbukumbu

Masama Blog akiwa na Malunde1 blog

 pozi tu
picha ya kumbukumbu,kushoto ni bwana Zainul Mzige
picha ya kumbukumbu

picha ya kumbukumbu

pozi flani hivi

picha ya kumbukumbu

picha ya kumbukumbu

Rose Ndauka,Mkala Fundikira na Joachim Mushi

Picha zote kwa hisani ya Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527