Ukatili!! MAMA AMKATA KATA VISU MWANAYE WA KUMZAA

 


Mtoto Christina Kusale (2) amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kufanyiwa ukatili na mama yake mzazi kwa kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali.
 
Amesema Ofisa Ustawi wa Jamii wa hospitali hiyo, Dk Rose Temu kuwa mtoto huyo ambaye anaishi Kinondoni alipelekwa na majirani baada ya kusikia akipigwa na mama yake.

Temu alisema waliingia ndani na kumkuta mtoto huyo akilia huku akiwa na majeraha yanayodhaniwa ya kisu na kumsababishia maumivu hayo.

“Mtoto Christina alifikishwa hospitalini hapa Februari 22, mwaka huu akiwa na majeraha mbalimbali kwenye mwili wake ambayo yalikuwa sehemu za usoni, mikononi, kwenye makalio, mapaja na mgongoni,” alisema Temu.

Alisema amelazwa wodi namba mbili akiendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Alisema mama wa mtoto huyo anashikiliwa na Polisi na uongozi wa hospitali unafanya utaratibu ili aende kwa ajili ya kuchunguzwa kama ana matatizo ya akili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527