Maajabu!! WANANDOA WAFARIKI DUNIA WAKIWA WAMESHIKANA MIKONO,WALIPENDANA SANA

shakingTumeshuhudia ndoa nyingi zikifungwa siku hizi lakini hazidumu, chache ambazo zimedumu ama zinadumu kwa muda mrefu.


Wanandoa hawa kutoka California, Marekani ambao walioana miaka 67 liyopita walikufa kwa kupishana saa chache wakiwa wameshikana mikono.

Floyd Hartwig mwenye miaka 90 na mkewe Violet mwenye miaka 89 wamefariki February 11 mwaka huu wakiwa nyumbani kwao baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Family photo of Floyd Hartwig and wife Violet who died hours apart while holding hands
Floyd Hartwig akiwa na mkewe Violet wakati wa ujana wao
“Walikua wakifurajia maisha yao kila siku,walipendana sana,walifanya kazi kwa kujituma na kuheshiamiana sana“alisema mmoja wa watoto wao Donna Scharton.

Kutokana na ukaribu wao familia hiyo baada ya kuwauguza kwa muda mrefu huku wakiwa wamewatengenishia vitanda baadaye waliamua kuwaweka pamoja.

Floyd ambaye alikua wa kwanza kufariki baada ya kusumbuliwa na kansa ya utumbo huku akiwa amemshika mkewe mkono na baada ya saa tano mkewe naye alifariki na kujikuta wote wakiwa wameshikana mikono pamoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527