SHUHUDIA HII KALI KUTOKA MTWARA!! WAZUNGU WAFANYIWA TAMBIKO,BAADA YA KUKUTANA NA MAUZA UZA

Bosi wa kampuni ya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd akinywa dawa ya tambiko
Bosi wa kampuni ya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd akipakwa dawa ya tambiko kwenye kipaji cha uso
Mabosi na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa katika tambiko hilo linalodaiwa kufanyika  wiki iliyopita.

Za kitaa kutoka Mtwara zinadai kuwa bibi mmoja aliyeitisha Serikali kuwa ikifanya mchezo na haki za watu wa mkoa huo atabadili gesi kuwa maji, amewapigia tambiko Wafaransa wazungu wa Kampuni ya uchimbaji wa visima vya mafuta ya Maurel et Prom (T) Ltd yenye ofisi zake Chole Road, Msasani Peninsular, Dar es Salaam, baada ya kile kilichodaiwa drill yao ya kuchimbia mafuta kukatika mara tatu wakati wakichimba kisima cha urefu wa mita 3,000 chini ya bahari.

  Inadaiwa baada ya kuanza kuona maajabu katika kazi yao hiyo, fasta walijisalimisha kwa bibi huyo huko Mtwara na kukubali kufanyiwa tambiko ili mambo yanyooke, kama wanavyoonekana pichani hapo juu! Kama ni kweli, basi bibi anatisha! Lol!!.
PICHA: Hisani ya Mtandao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527