KIGOGO ALIYETAKA KUMUUA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM ABURUZWA MAHAKAMANI


Mshauri wa masuala ya ulinzi katika Benki Kuu (BoT), Shaban Ndosi (39) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kujaribu kumuua ofisa wa Polisi.

Ndosi alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema. 
 
Wakili wa Serikali, Janeth Kitali alidai kuwa Oktoba 21, 2014 katika eneo daraja la Salender karibu na mataa ya kuongoza magari, alijaribu kumuua askari Polisi, Koplo Salehe.
 
Hakimu Lema alisema mshitakiwa hatakiwi kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na upelelezi umeshakamilika hivyo kesi itahamishiwa Mahakama  Kuu.
 
Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika waliosaini hati ya dhamana ya Sh milioni mbili pia alitakiwa kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria. Kesi hiyo itatajwa tena Februari 23 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527