HILI NDIYO KUBWA ZAIDI KUTOKA SHINYANGA LEO-BONGO MOVIE SHINYANGA YAWAPIGIA FILIMBI WASANII


Katibu wa Bongo Movie Shinyanga Sophia Kichochi akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao zilizoko Ngokolo karibu na Moleka Hotel ambapo amewataka wakazi wa Shinyanga kuanzia umri wa miaka 12 kujitokeza kujiunga na umoja wa wasanii wa filamu Tanzania (Bongo Movie Tawi la Shinyanga) lililofunguliwa rasmi kwa kikao kilichofanyika jijini Mwanza tarehe 22/6/2014 ambapo mgeni rasmi wa mkutano huo alikuwa Mheshimiwa waziri Bernard Membe

Kichochi alisema Bongo Movie Shinyanga ambayo mwenyekiti wake ni Juma Ibrahimu Songoro maarufu kwa jina la Songoro inalenga kuleta mabadiliko ya wasanii na umoja na maendeleo Tanzania

Miongoni mwa malengo ya Bongo Movie Shinyanga ni Kujikwamua kiuchumi kwa kutafuta ajira kwa vijana kwa kutumia vipaji vyao vya sanaa ya kuigiza
,Uigizaji wa filamu na maonyesho,
Uandaaaji wa matamasha ya kisanii na kuweza kufikisha ujumbe mbalimbali za kitaifa kupitia sanaa ya uigizaji n.k


Aliyataja masharti ya anayetaka kujiunga uanachama Bongo Movie Shinyanga kuwa na sifa hizi: Awe na akili timamu,awe anajua kuigiza,hakuna kigezo cha umri wala jinsia,awe mhuzuriaji wa vikao vinavyoandaliwa na bongo movies,awe mwenye kujituma,awe aliyetimiza haya masharti na kujaza fomu na kitambulisho,lakini pia awe na picha tatu za paspot size na atimize gharama za usajili zifuatazo ikiwemo fomu ya kujiunga,ada,na kiingilio vyote vikiwa na gharama isiyozidi shilingi elfu 30.
 Ofisi zao zipo Ngokolo mjini Shinyanga karibu na Moleka Hotel ukifika hapo utaona Maandishi yanayosomeka Bongo Movies Development Organization(B.D.O) Shinyanga .TZ.Kama una kipaji Wasiliana nao kwa Email
Bongomovieshy05@gmail.com, au wapigie simu namba zinazosomeka hapo juu au chini au fika kwenye ofisi zao

 Maandishi yanayosomeka kwenye ofisi za Bongo Movie Shinyanga
Katibu wa Bongo Movie Shinyanga Sophia Kichochi akizungumza na waandishi wa habari leo

Picha ya pamoja baadhi ya wanachama wa Bongo Movie Shinyanga na waziri Membe wakati wa uzinduzi wa Bongo Movie Shinyanga jijini Mwanza tarehe 22/6/2014

Mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga Juma Ibrahimu Songoro maarufu kwa jina la Songoro


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527