Hii Kali!! AAMUA KUTEMBEA NA SHELA MTAANI KUWAPINGA WANAOMSEMA KACHELEWA KUOLEWA!!

salma 2
Mwanamke mmoja nchini Misri ameamua kukatiza na gauni la harusi mitaani kupinga masimango anayokutana nayo kwa kuchelewa kuolewa.
Samah Hamdi mwenye miaka 27  alifikia uamuzi huo baada ya kuchoshwa na kashfa kutoka kwa watu wanaomzunguka ikiwemo familia yake hasa mama yake mzazi ambao wamekua wakimsema  kutokana na kutokua na mume mpaka sasa.
salma4
Hamdi ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili alisema ameamua kutembea hivyo mitaani  na kamwe hawezi kuacha dhamira yake hiyo ikiwa kama ishara ya kupinga mila na desturi inayowakandamiza wanawake wasioolewa.
salma
Samah Hamdi akiwa anatafakari jambo huku akiwa amevaa gauni lake la harusi katika moja ya mitaa jijini Cairo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527