BAADA YA PROF MUHONGO KUJIUZULU!! RAIS KIKWETE ATEUA MAWAZIRI WAPYA 13,ORODHA IKO HAPA,TAYARI WAMEAPISHWA JIONI HII

 
Saa chache tu baada ya Profesa Sospeter Muhongo waziri wa nishati na madini wa Tanzania kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na sakata la Escrow,rais Kikwete amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Jioni hii Ikulu imefanya mkutano wa ghafla na waandishi wa habari,uliofanyika ikulu jijini Dar es salaam

Hawa ndiyo Mawaziri 8 walioteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete leo
 
1.George Simbachawene- Waziri wa Nishati na Madini
2.Mary Nagu -Waziri wa nchi Mahusiano na Uratibu
3.Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
4.Wiliam Lukuvi - Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
5.Steven Wassira - Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
6.Samwel Sitta - Waziri wa Uchukuzi
7.Jenista Mhagama - Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge
8.Christopher Chiza- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji


Manaibu Waziri  5 walioteuliwa
1.Steven Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
2.Angellah Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi
3.Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4.Anna Kilango- Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5.Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini


Nafasi ya Profesa Sospeter Muhongo aliyekuwa waziri wa nishati na madini imechukuliwa na George Simbachawene huku nafasi ya Profesa Anna Tibaijuka aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikichukuliwa na William Lukuvi.


 Charles Mwijage sasa ni naibu Waziri wa Nishati na Madini akichukua nafasi ya Steven Masele ambaye sasa ni
naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano  


Rais Kikwete amewaapisha  mawaziri na manaibu waziri wapya ikulu jijini Dar es salaam kuanzia saa 18:10hrs amemaliza saa 18:40hrs kisha zoezi la kupiga picha za pamoja na wateule hao likaendelea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527