UTATA WA KIFO CHA MSANII AISHA MADINDA_MAZISHI YAAHIRISHWA POLISI WACHUNGUZE

Taarifa za mazishi ya mnenguaji maarufu kwenye familia ya muziki wa dansi Tanzania Aisha Mohamed Mbegu maarufu kama ‘Aisha Madinda’ zimeahirishwa kutokana na upelelezi wa Polisi unaoendelea juu ya kifo cha marehemu kwani kumekuwa na utata juu ya kifo cha mwanadada huyo kilivyotokea.
ALIYEKUWA mnenguaji na mwimbaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda aliyefariki jana asubuhi, atazikwa kesho mchana badala ya leo kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

Mtoto wa kwanza marehemu, Feisal amesema kuwa polisi wamesema ni lazima mwili wa mama yake ufanyiwe upasuaji (postmortem) ili kujua chanzo cha kifo chake.

Awali ndugu wa marehemu walisema hawahitaji Asha Madinda afanyiwe upasuaji, lakini baada ya polisi kutembelea eneo la tukio la kifo chake huko Mabibo, wamesema ni lazima upasuaji ufanyike.


Feisal amesema upasuaji unatarajiwa kufanyika leo mchana hali inayowalazimisha kubadili ratiba ya mazishi. Aisha Madinda sasa atazikwa kesho mchana baada ya sala ya Ijumaa.


Pichani Marehemu enzi za uhai wake akiwa na watoto wake kushoto ( Feysal Madinda na wa kike Neyma Madinda

Feysal Madinda ambaye ni mtoto wa marehemu Dec 18 amepost ujumbe kwenye instagram na kuandika taarifa za kuahirishwa kwa mazishi ya mama yake Aisha Madinda ikiwemo na siku atakayozikwa endapo upelelezi utakapokamilika. 

"INNALILLAH WAINNALILLAH RAJUUUUN, NAAAAMINI DUNIANI TUNAPITA MBELE YEYE NYUMA SISI… NINGE PENDA KUTOA SHUKLAN ZANGU ZA ZATI KATI YA NDUGU JAMAAA NA MALAFIKI KWA UKARIMU MLIO UWONESHA MPAKA TYM IZI…. NILITEGEMEA TUNGEMZIKA LEO MALEHEM LAKIN IMEKUA NGUMU KUTOKANA NA SABAB ZILIZO NNJE YA UWEZO, SAMAHANINI SANA KWA USUMBUFU ULOJITOKEZA MANA KUNA WENGI WALIKUA WANAJUA TUNAZIKA LEO, NINGEPENDA SEMA KUWA TUTAMPUMZISHA KESHO BAAAADA YA SALA YA IJUMAAA NA BAAAADA YA UCHUNGUZI KUKAMILIKA…. MSIBA UPO KIGAMBONI MAENEO YA MIKADI BEACH NA MAZISHI YATAFANYIKA IO KESHO PANAPO MAJALIWA SAA 7 MCHANA #ASANTENI_SANA"



Mpenzi Msomaji,Tunapenda kukutumia Habari zetu zote mara tu Tunapoziweka Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527