BAJAJI YA CHADEMA YAITUNGUA CHOPA YA CCM HUKO GEITA,MKASA MZIMA UKO HAPA



Kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Musukuma akiwaonyesha dole gumba wananchi wa mtaa wa Nyankumbu Geita muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa alipowasili Geita na naibu katibu mkuu wa CCM taifa Mwigulu Nchemba kuongeza nguvu katika kampeni hivi karibuni-Picha na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita

Hivi karibuni_Aliyekaa mbele ni katibu wa CDM jimbo la Geita Mutta Robert akiwa amekaa kwenye bajaji iliyokuwa inatumiwa na CDM kama usafiri kufanya kampeni na matokeo yake, kukigalagaza Chama Cha Mapinduzi kilichokuwa kinatumia usafiri wa helikopta kufanya kampeni zake-Picha na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita


Chama cha demokrasia na maendeleo (chadema)jimbo la Geita kilichofakuwa kikifanya kampeni zake kwa kutumia usafiri wa pikipiki ya miguu mitatu(bajaji)kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye halmashauri ya mji wa Geita na kukishinda chama cha mapinduzi (CCM)ambacho kilikuwa kikifanya kampeni zake kwa kutumia usafiri wa helkopita(CHOPA)ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Musukuma.


Katika uchaguzi huo,mbali na kasoro nyingi zilizojitokeza ikiwemo mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita kudaiwa kukibeba Chama Cha Mapinduzi,halmashauri ya mji wa Geita yenye mitaa 65,Chadema imejizolea mitaa 33,cuf mtaa 1 na ccm mitaa 18,ambapo katika mitaa hiyo,mitaa 3 ccm waliipata kwa kuweka pingamizi kwa wagombea na kuondolewa huku mitano ikishindwa kushiriki kutokana na sababu mbalimbali.

Hata hivyo baadhi ya wananchi katika Halmashauri ya mji Geita wamemtaka Waziri wa tawala za mikoa na Serikali za  mitaa Hawa Ghasia kumchukulia hatua kali mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Magreth Nakainga kwa kuvuruga na kuchakachua matokeo ya uchaguzi wa mitaa katika mji wa Geita.

Mkurugenzi huyo anatuhumiwa kuingilia baadhi ya vituo vya kupigia kura na kufuta matokeo na kutangaza uchaguzi urudiwe baada ya kugundua wagombea wa CCM wameshindwa katika matokeo hayo.


Hata hivyo mbali na uchakachuaji huo,mji wa Geita wenye mitaa 65,Chadema imejizolea mitaa 33,cuf mtaa 1 na ccm mitaa 18,ambapo katika mitaa hiyo,mitaa 3 ccm waliipata kwa kuweka pingamizi kwa wagombea na kuondolewa huku mitano ikishindwa kushiriki kutokana na sababu mbalimbali.


Mitaa ambayo mkurugenzi huyo alitangaza matokeo kinyume na kanuni za uchaguzi ni pamoja na mtaa wa Elimu, Mission na Katoma.

Matokeo ya mtaa wa Katoma yalikuwa ni mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) alishinda kwa kura 428 tofauti kubwa ya kura dhidi ya mgombea wa chama cha mapinduzi (ccm) aliyepata kura 364.

Mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) ni Patrick Faida na mgombea wa chama cha mapinduzi (ccm) ni Aloyce Bayona 

Aidha mtaa mwingine ambao inadaiwa mkurugenzi huyo alitangaza matokeo kwa kutumia jeshi la polisi ni mtaa Elimu kata ya Nyankumbu mjini Geita ambapo wapiga kura walikuwa wameisha vamia kituo cha kupigia kura na kuvunja masanduku ya kura,kuchana karatasiza kura na msimamizi msaidizi kukimbia.

Baada ya mkurugenzi kupata taarifa ya kituo kuvamiwa na wapiga kura kwa madai kwa msimamizi msaidizi kudai kura zimezidi idadi ya waliopiga kura,mkurugenzi alifika akiwa na polisi wapatao wane na kutangaza kuwa mgombea wa chama cha mapinduzi ameshinda.

Katibu wa chadema Jimbo la Geita,Mutta Robert,alisema kuwa kulikuwa na njama za kuhakikasha mitaa yote ya Halmashauri ya mji wa Geita inatangazwa matokeo yake kwa ubabe kwa kutumia jeshi la Polisi ili kuisaidia ccm.

“Tulipata taarifa mapema kwamba mkurunzi wa mji wa Geita kwa kushirikiana na CCM wamepanga kutumia polisi kutangaza matokeo ya mitaa kwa nguvu baada ya kubaini kuwa chadema itashinda mitaa mingi”,aliiambia Malunde1 blog

“Tuliimarisha ulinzi kwa kutumia  brigedia nyekundu  ya ulinzi ya chama chetu na kuwaelewa wapiga kura wetu mapema njama za ccm za kutaka kuiba kura kwa kutumia polisi,wapiga kura waliakikisha wamepiga na kulinda kura zao.”

Alisema kuwa baadhi ya vituo ambavyo wapiga kura walijisahau kidogo mkurugenzi huyo alitumia nafasi hiyo kutangaza mgombea wa chama cha mapinduzi.

Robert alisema kuwa mtaa wa Mission na mtaa wa Elimu idadi ya kura zilizokuwa kwenye sanduku la kura zilizidi idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura na mkurugenzi huyo alitangaza matokeo na kuwapa ushindi wagombea wa chama cha mapinduzi,lakini mtaa wa Katoma ambao idadi ya kura ilizidi wapiga kura na mgombea wa chadema kushinda,mkurugenzi huyo alifuta matokeo. 

“Huyu mkurugenzi alikula njama mapema, maana mitaa yote 60 ya Halmashauri ya mji wa Geita ilikuwa na karatasi pungufu na sehemu nyingine  nilipompigia simu kumweleza mapungufu hayo alipeleka karatasi za kura baada mawili kupita na alipokuwa akipeleka zingine zilikuwa zinakuwa za kituo tofauti na hicho” alisema Robert.

Mkurugenzi alisema kuwa hayo ni matatizo madogo madogo yaliyotokea nchi nzima na sio kwenye Halmashauri yake tu na hakutegemea kama wapiga kura watakuwa  wengi ndiyo maana alikuwa anapeleka karatasi chache chache vituoni.

Kuhusu madai ya Katibu wa chadema Mutta Robert kuwa mkurugenzi alikuwa na njama na ccm na kutangaza matokeo kibabe alisema ,

 “Hivi huyu kijana kwa chadema ni nani? Ni msumbufu sana lakini inaonekana anajaza mambo yasiyo ya kweli”.

Mji wa Geita una mitaa 65 lakini iliyoshiriki uchaguzi huu ni 60 na kati ya hiyo,Chadema imejizolea mitaa 33,cuf mtaa 1 na ccm mitaa 18 lakini mitaa 3 ccm waliipata kwa kuweka pingamizi kwa wagombea na kuondolewa.

Hivyo kwenye matokeo ya kupigiwa kura,ccm imepata mitaa16 tu na mitaa 4 uchaguzi wake unafanyika jumapili wiki hii ambapo chadema inaonekana kuwa na ushawishi mkubwa katika mitaa hiyo.Mitaa hiyo ni Katoma,Nyerere road,Mwatulole na Lwenge.

Malalamiko haya yanakuja siku moja baada ya waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa Hawa Ghasia kutangaza kuwa mtumishi wa serikali yeyote aliyeshiriki kuharibu uchaguzi huu atashughulikiwa na kuwajibishwa mara moja na tayari wengine wameshaanza kuwajibishwa .
Na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita

Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527