MNENGUAJI MAARUFU MUZIKI WA DANSI AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA,KIFO CHAKE CHADAIWA KUWA NA UTATA



Taarifa tuliyoipata mchana huu ni kuhusu kifo cha aliyekuwa Mnenguaji maarufu kwenye familia ya muziki wa dansi Tanzania Aisha Mohamed Mbegu maarufu kama ‘Aisha Madinda’.

Aliyekuwa mnenguaji wa bendi tofauti hapa nchini Tanzania Aisha Madinda amefariki dunia na mwili wake wakutwa umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.


Akiongea na EATV Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta amesema kuwa alipewa taarifa na Daktari mmoja kuwa wameona kama mwili wa Aisha Madinda hospitalini hapo, ndipo akatuma watu kwenda kuangalia akiwemo Luiza Mbutu ili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndipo walipogundua ni yeye.

“ Mimi nipo njiani natoka Kigoma kuja Dar es Salaam, ni habari ya kusikitisha sana maana Aisha amefariki katika mazingira ya kutatanisha sana, jana alikuwa mzima na anachati na watu kwenye simu leo napigiwa simu mwili wake umekutwa umehifadhiwa kwenye hospitali ya Mwananyamala, hata sielewi nini kimetokea”. Amesema Asha Baraka

Picha za Aisha akiwa kazini enzi za uhai wake

aishamadinda

Mungu ailaze roho ya Marehemu Aisha Madinda mahali pema peponi , Amina

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527