PICHA AJALI YA COSTA ILIYOUA WATU 11 NA KUJERUHI 25 HUKO TANGA,DEREVA ALIKUWA ANASINZIA BARABARANI

Costa ikiwa imeharibika 

IMG-20141127-WA0016
Eneo la tukio
IMG-20141127-WA0015
Watu 11 wamekufa na wengine 25 kujeruhi vibaya baada ya basi dogo aina ya Coaster la kampuni ya ''Thende Sheki'' kugongana uso kwa uso na lori la mizigo katika eneo la mkanyageni lililopo wilayani Muheza mkoani Tanga.

Ajali hiyo ilikusanya mamia ya wananchi kutoka jijini Tanga,muheza na lushoto kwa ajili ya kwenda kushuhudia na kutambua miili ya marehemu iliyokuwa imehifadhiwa nje katika hospitali teule ya mtakatifu augustino wilayani muheza kwa ajili ya utambuzi ambapo hadi majira ya mchana miili ya watu 9 waliokufa papo hapo katika eneo la tukio ilitambuliwa na ndugu na jamaa.

Akielezea miili na majeruhi waliopokelewa katika hospitali hiyo,kaimu mganga mkuu wa wilaya ya muheza Dkt.Perter Shemkhai amesema watu wawili walifariki hospitali muda mchache baada ya kuletwa na kupatiwa tiba katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamesema dereva mwenye lori alikuwa akiyumba njia nzima kabla ya kukutana uso kwa uso na gari dogo la abiria aina ya Coaster hatua waliyodai kuwa ina viashiria vya dereva wa lori hilo alikuwa amepitiwa na usingizi wakati akiwa barabarani. 

BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527