MJADALA WA ESCROW HALI TETE, SASA KUFANYIKA LEO JIONI BAADA YA KUAHIRISHWA ASUBUHI


Mjadala wa Ripoti ya CAG Kuhusu Akaunti ya Escrow hali tete Bungeni Mjini Dodoma.


Wabunge wote wameshinikiza mjadala huo kusomwa lakini Mwenyekiti wa Bunge, Mbunge wa Ilala Mheshimiwa  Mussa Zungu Azan ameahirisha Bunge mpaka saa kumi na moja jioni.

Utata ulianza mara ya kipindi cha maswali na majibu ambapo wabunge wengi kutoka vyama mbalimbali vinavyounda Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliposimama kuomba Muongozo.

Karibu wabunge wote Muongozo wao ilihusu kusomwa kwa Ripoti ya Akaunti ya Escrow.

Mwenyekiti wa Bunge Mh Zungu alinukuliwa akisema amepokea miongozo hiyo na kwamba wabunge walioomba Muongozo watajibiwa jioni, ndipo mweyekiti wa Bunge hilo Mh Zungu alipotangaza kusitisha shuguli za bunge mpaka saa kumi na moja jioni ya leo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527