MTOTO AFARIKI BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA KIREFU KILICHOPO SHULENI MJINI SHINYANGA,PICHA ZIKO HAPA

 BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 

Mwili wa mtoto Mack Johnson ukitolewa kwenye kisima cha maji na wananchi waliofika eneo la tukio wakishirikiana na jeshi la wananchi na jeshi la zimamoto na uokoaji.Mtoto huyo (5)alikuwa anasoma darasa la awali katika shule ya Sheer Bliss amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji chenye urefu wa futi 50 kilichopo eneo la shule mtaa wa Majengo Mapya katika manispaa ya Shinyanga.

 Kisima chenye urefu wa futi 50 ambapo mtoto Mack amefariki dunia baada ya kutumbukia,ngazi mbili za jeshi la zimamoto pamoja na kuungwa pamoja lakini hazikuweza kufikia kina cha kisima hicho na badala yake ikatumika kamba ndefu na mmoja wa wananchi kujitoa mhanga kutumbukia nayo kisimani kuutoa mwili wa mtoto huyo.

Mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea leo  saa tatu  asubuhi ambapo mtoto huyo alitumbukia kwenye kisima hicho wakati akicheza na wenzake karibu na kisima hicho kilichopo eneo la shule ambacho kimefunikwa na makaravati yaliyoonekana kuchakaa.
Kamba ikiwa ndani ya kisima ikiwa imeshikiliwa kwa nje na wananchi huku ndani akiwemo mmoja wa wananchi hao aliyeingia na kamba hiyo kuokoa maisha ya mtoto ndani ya kisima.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa eneo la tukio Dkt  Anselm Tarimo amesema  wamebaini kuwa mazingira ya shule hiyo siyo rafiki, shimo lilikuwa halijafunikwa hivyo kuwaomba wataalam mbalimbali wawe wanapita katika maeneo wanakosomea watoto ili kujua mazingira ya watoto kuepusha majanga yanayoepukika.

 BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527