Inatisha!! BIBI HARUSI AUA MME WAKE KWA KUMNYWESHA SUMU YA PANYA SIKU YA HARUSI



Tunataka Tukutumie Habari zetu mara tu Tunapoziweka Mtandaoni,Bonyeza Hapa
Msichana mdogo aliyeolewaBi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za harusi yake.

Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu.
Wasila Tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa.
Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama Hamziyya,ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi harusi huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho.
Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi zimekithiri.
Msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba Tasi'u alimpa fedha ili kununua sumu ya panya kutoka duka moja jirani mnamo tarehe 5 mwezi Aprili,siku ambayo bwana Sani alifariki.
''Alisema kuwa panya wanamsumbua katika chumba chake'',Hamziyya aliiambia mahakama.
Upande wa mashtaka baadaye ulisema kuwa badala yake Tas'u aliweka sumu hiyo ya panya katika chakula ambacho alikuwa amekiandaa kwa sherehe za baada ya harusi kwa kuwa alijuta uamuzi wake wa kumuoa bwana Sani.
Msichana huyo alikataa kuzungumza mahakamani.
Jaji Mohammed Yahaya,katika mahakama ya Gezawa alitoa hukumu kwamba Tasi'u ambaye alikataa kuongea katika mahakama hana hatia katika kusikizwa kwa kesi mnamo mwezi Octoba ambapo alisomewa mashtaka.
Jaji huyo alikataa ombi la upande wa mshtakiwa la kesi hiyo kupelekwa katika mahakama ya watoto.
Ushahidi wa Hamziyya uliungwa mkono na Abuwa Yussuf muuzaji duka katika mji wa Unguwar Yansoro ambaye alithibitisha kuuza sumu hiyo kwa mtoto huyo.
Jirani ya Bwana Sani mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkulima, Abdulrahim Ibrahim alitoa ushahidi ambapo alisema kwamba alipewa chakula hicho kilichopikwa na Tasiu.
''Nilipoletewa chakula hicho niliona vipande vipande vyeusi''aliiambia mahakama.
Alikula vipande vinne vya madonge vilivyotengezwa na maharagwe lakini hakupendelea ladha yake'',alisema na kuongezea kuwa ni Umar pekee aliyeendelea kula.
Baadaye alisema kuwa alimuona bwana Sani katika bustani ,akiwa mgonjwa na kumpeleka nyumbani.
Lakini alipokuwa akijaribu kumuuguza bwana sani ,aligundua kwamba watu wengine watatu ambao walikuwa wamekula chakula hicho wamefariki ghafla.
Viongozi wa mashtaka walidai kwamba chakula cha Tasiu kilichowekwa sumu kiliwaua watu wanne na hivyobasi kuwajumuisha wanne hao katika kesi moja ya mauaji.
Nigeria haijawahi kumyonga mtoto aliyefanya uhalifu tangu mwaka 1997,ambapo taifa hilo liliongozwa na dikteta Sani Abacha,kulingana na shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch.
via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527