HIKI NDICHO KIMETOKEA BAADA YA MWANAMKE ALIYEVAA NUSU UCHI KUVULIWA NGUO HUKO KENYA


Na wanaume walikuwepo kuwaunga mkono wanawake katika maandamano yao
Maandamano hayo yamefanyika chini ya kauli mbiu 'My dress my choice'
Wanawake mjini Nairobi, Kenya leo wameandamana kupinga kitendo cha mwanamke mmoja kuvuliwa nguo wiki jana kwa madai kuwa
alikuwa amevalia sketi fupi sana.
Wanawake wengi walikerwa na kitendo hicho wakisema kuwa kila mwanamke ana haki ya kuvalia mavazi yanayomfurahisha.
Hiyo wiki jana kanda ya video ilisambazwa kwa mitandao ya kijamii ikionyesha mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina hadi sasa akivuliwa nguo zake na wanaume katika kituo cha magari ya abiria kati kati mwa Nairobi.
Wanawake mashuhuri wakiwemo wasanii, wanasiasa na wanaharakati walilaani kitendo hicho wakihoji kwani mavazi ya mwanamke yanamhusu nini mwanamume ambaye sio mumewe wala jamaa yake.
Baadhi walikitaja kitendo hicho kuwa cha kinyama na kinachokiuka haki za wanawake.
Msanii mmoja mashuhuri Nyota Ndogo alinukuliwa akisema ikiwa wanaume wanawavua nguo wanawake kwa kile wanachosema ni mavazi yasiyo ya kiheshima, basi na wanaume wanaolegeza long'i zao na wao basi pia wavuliwe nguzo zao.

<<BONYEZA MANENO HAYA TUKUTUMIE PICHA ZA VITUKO NA VICHEKESHO>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527