HIACE YA KAHAMA-SHINYANGA YAUA WATU WENGI KONA YA BUHANGIJA MJINI SHINYANGA

BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 
Hiace iliyopata ajali ikiwa eneo la tukio huku ikiwa imeharibika vibaya-Picha na Kadama Malunde

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde

Gari ikiondolewa eneo la tukio

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo akiwa na maafisa wa polisi mkoa wa Shinyanga eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde
Watu tisa wamepoteza maisha  leo majira ya saa nne na nusu asubuhi baada ya gari ndogo Hiace yenye namba za usajili T761 CKD ikitoka Kahama kwenda Shinyanga Mjini kupinduka katika eneo la Kona ya Buhangija mjini Shinyanga barabara ya Tinde-Shinyanga.

Walioshuhudia wanasema hiace hiyo ilikuwa katika mwendo kasi ikifukuzana na Hiace nyingine ndipo ikamshinda dereva wake baada ya kupiga Bamz ya Buhangija na kupinduka mara tatu kisha kutumbukia mtaroni.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema wameondoa miili mitano ya marehemu katika gari hiyo.

Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga na wanaendelea na matibabu.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum amesema wamepokea miili mitano ya marehemu,na wengine wamefariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo

 Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Longinus Tibishubwamu abiria waliofariki ni 9 na majeruhi wako 9.

Amesema gari lililopata ajali ni mali ya Fabian Mzaya wa Shinyanga ilikuwa  ikiendeshwa na Anuari Awadhi mkazi wa wa Shinyanga aliyekimbia baada ya ajali kutokea

SOMA HABARI KAMILI HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527