ANGALIA PICHA_HII HAPA TAARIFA KAMILI KUHUSU AJALI YA HIACE ILIYOUA NA KUJERUHI BAADA YA KUPARAMIA TUTA NA KUPINDUKA SHINYANGA

BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 
Hiace yenye namba za usajili T761 CKD ikiwa imepinduka baada kuparamia tuta la barabarani na kupoteza mwelekeo kisha kutumbukia mtaroni katika eneo la Buhangija mjini Shinyanga barabara ya Tinde-Shinyanga leo saa nne na nusu asubuhi-Picha na Kadama Malunde

Gari hilo likiwa limeharibika vibaya-Picha na Kadama Malunde

Mashuhuda wakiongea na waandishi wa habari,ambapo walisema dereva alikuwa anafukuza na hiace nyingine huku akipisha gari jingine alipofika kwenye tuta gari ikamshinda,ikapinduka mara 3,ikagonga daraja kisha kutumbukia mtaroni-Picha na Kadama Malunde

Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema wamepokea miili mitano ya watu waliofariki dunia papo hapo eneo la tukio na wengine walifariki wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo na kwamba majeruhi 9 wanaendelea kupatiwa matibabu-Picha na Kadama Malunde

Ndani ya wodi namba 5 walikolazwa baadhi ya majeruhi.Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Longinus Tibishubwamu anasema watu waliopoteza maisha ni 9,majeruhi ni 9-Picha na Kadama Malunde

Majeruhi akipatiwa matibabu-Picha na Kadama Malunde

Majeruhi akiwa wodini akipatiwa matibabu-Picha na Kadama Malunde

Majeruhi Emmanuel John aliyekuwa anatoka Mwakitolyo kwenda Mwanza na gari hiyo iliyokuwa inaishia mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde

Majeruhi Katumbi Nangi akiwa nje ya wodi namba 5 aliyekuwa anasafiri kutoka Ulowa akizungumza na waandishi wa habari-Picha na Kadama Malunde

Majeruhi akiwa ndani ya wodi namba 7,hatukupata jina lake-Picha na Kadama Malunde

Majeruhi Flora Ngudungi aliyekuwa anasafiri kutoka Kahama kwenda mjini Shinyanga akiwa amelazwa katika wodi namba 7 katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga-Picha na Kadama Malunde

Majeruhi akiwa wodini(hatukupata jina lake)-Picha na Kadama Malunde

Majeruhi akiwa wodini(hatukupata jina lake)-Picha na Kadama Malunde

<<MAJINA YA WALIOFARIKI NA MAJERUHI YAKO HAPA>>
BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527