Kimenuka!! MAKAHABA NA WATEJA WAO WAPEWA "MASAA 48" KUSITISHA BIASHARA HIYO



Katibu wa maendeleo ya jamii katika jiji la Abuja Nigeria, ametangaza ‘kiama’ kwa wanawake wanaofanya ‘biashara ya kujiuza’ pamoja na wateja wao.
Taarifa iliyochapishwa na Today Internet Newspaper imesema, katibu mkuu huyo Blessing Unoh amesema serikali imetoa amri ya kusitisha biashara hiyo ndani ya saa 48, kwa yeyote atakayekiuka hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Amri hiyo imetolewa saa chache baada ya katibu mkuu huyo kutembelea maeneo mbali mbali ambayo yamebobea kwa biashara hiyo ambapo amejionea hali halisi iliyopo.
Aidha amesema kwa yeyote atakeyekiuka amri hiyo na kukutwa na hatia ya kutenda kosa hilo awe tayari kukabiliana na hukumu ya kifo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527