Inatisha!! MGANGA WA JADI ANASWA NA BUNDUKI ZIKIWA ZIMEFUNGWA HIRIZI NA NGOZI YA MNYAMA HUKO KAHAMA-SHINYANGA


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus  Kamugisha

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia mganga wa kienyeji bwana Mtabanzila Buyiyi(70)mkazi wa mtaa na kata ya Malunga wilayani Kahama kwa kosa la kukamatwa akiwa na bunduki mbili aina ya gobore zisizokuwa na namba zikiwa na hirizi akimiziliki kinyume cha sheria.

Malunde1 blog inaarifiwa kuwa tukio hilo limetokea juzi saa tano na dakika 41 asubuhi wakati askari polisi wakiwa doria na msako katika kata ya Malunga wilayani Kahama na kufanikiwa kukamata bunduki mbili  aina ya gobore zisizokuwa na namba zikiwa zimefungwa hirizi na vipande vya ngozi ya mnyama asiyefahamika katika nyumba ya mganga huyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus  Kamugisha amesema bunduki hizo zilikuwa zinamilikiwa kinyume cha sheria na zinadaiwa kutumika kufanya matukio ya uhalifu sehemu mbalimbali za mkoa wa Shinyanga.

Aidha amesema pia wanamshikilia mtoto wa mganga huyo bi Nyamisi Mtabanzila(40) kwa kosa la kuendesha shughuli za uganga na baba yake bila leseni.

Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527