Breaking News!!! KIWANDA CHA MAGODORO KILICHOPO BARABARA KUU YA MWANZA-SHINYANGA CHAUNGUA MOTO

Habari zilizokifikia chumba cha habari cha Malunde1 blog hivi punde ni kwamba Kiwanda cha magodoro cha Vitanda Manufacturing cha Mwanza kilichopo eneo la Mkuyuni kando ya barabara kuu ya Mwanza Shinyanga kimeungua na kuteketea kwa moto.

Moto huo ambao unadai kuzuka majira ya saa 1: 46 usiku huu unadaiwa kuanzia katika ghala na kisha kushika matika ya yaliyokuwa na Tindikali.


Inalezwa kuwa moto huo umeteketeza sehemu ya ghala hilo na jitihada za kuuzima zinaendelea usiku huu.
Mpaka majira ya saa 8:55 hali ilikuwa mbaya kutokana na kuwasili kwa gari moja la zimamoto ambalo lilionekana kuzidiwa nguvu na moto huo kutokana na kuwa na uwezo mdogo.

<<BONYEZA MANENO HAYA KUANGALIA PICHA KIWANDA KIKIUNGUA MOTO>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527