BASI UNAAMBIWA MATAULO YANASAMBAZA VIRUSI VYA UKIMWI,SOMA HAPA

Kituo kimoja cha televisheni nchini Marekani kinachorusha kila siku kipindi cha mhubiri Pat Robertson kiliomba radhi Jumatatu kwa madai yake potofu kwamba wasafiri wanaokwenda Kenya wanaweza kupata maambukizi ya Ukimwi kwa njia ya taulo.
 Dr Robertson alikosea kusema juu ya uwezekanao wa kupata Ukimwi kwa njia ya mataulo
kimesema kituo cha Utangazaji cha Kikristo, CBN, katika mtandao wa Facebook.
 CBN imegundua mara moja kosa hili na kuondoa kauli hiyo kutoka kwa maktaba ya mtandao huo. CBN inaomba radhi kwa mkanganyiko wowote.
Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 84, mwinjilisti mkongwe ameonya katika kipindi chake cha "700 Club" cha Oktoba 16 kwamba wasafiri watalazimika kuchukua tahadhari ya hali ya juu ya kiafya wawapo nchini Kenya.
 Unaweza kupata Ukimwi nchini Kenya
Bwana Robertson aliwaambia watazamaji wake wanaokadiriwa kufikia milioni moja. Watu wana ukimwi. 
 Unatakiwa kuwa makini. Nina maana kuwa, mataulo yanaweza kuwa na virusi vya Ukimwi.
Madai ya Bwana Robertson haraka yalishambuliwa na makundi yanayojihusisha na masuala ya ugonjwa wa Ukimwi.
Wamesema kuwa Ofisi ya serikali ya Marekani ya Masuala ya Afya ya kina Mama inasema virusi vya Ukimwi haviwezi kuambukiza kwa njia ya 
 kushirikiana vyombo vya chakula, mataulo na mashuka, simu au vyoo .
Matamshi ya Bwana Robertson yamekuja kutokana na swali alilotumiwa kwa njia ya barua pepe na mtu asiyejulikana ambaye alielezea wasiwasi juu ya madhara ya kutembelea Kenya wakati wa mlipuko wa Ebola barani Afrika.

Alimhakikishia mtazamaji wa kipindi chake kuwa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini Kenya akisema Kenya iko mbali na kitovu cha mlipuko wa Ebola, Afrika Magharibi.

Lakini Bwana Robertson alieleza hatari ya kuambukizwa magonjwa mengine nchini Kenya pamoja na Ukimwi.

Mbu wanaweza kusababisha madhara makubwa ya ugonjwa, amesema, akiongezea kwamba
usafi akielezea kuwa tatizo lingine. Unakunywa maji, hayajachujwa, unaweza kupata ugonjwa wa matumbo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527