TRAFIKI AGONGWA AKIWA KAZINI BAADA YA KUSIMAMISHA GARI GHAFLA

WP 2806 CPL Riziki, akiwa chini baada ya kugongwa na daladala eneo la Mbagala Rangi 3 jana kabla ya kukimbizwa hospitali.

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kituo cha Mbagala wilayani Temeke, Koplo Riziki Mohamedi amelazwa katika Hospitali ya Rufani ya Muhimbili baada ya kugongwa na gari akiwa kazini eneo la Mbagala rangi tatu jijini Dar es salaam
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyekataa kutajwa jina alidai kuwa trafiki huyo alisimamisha gari ghafla na gari la nyuma lililokuwa nyuma likapita bila kusimama na kumgonga na kisha kuyagonga magari mengine yaliyokuwa mbele.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya Kihenya alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea asubuhi eneo la Mbagala Rangitatu.
Alisema gari aina ya Toyota Hiace inayofanya safari zake kati ya Temeke na Kongowe lilishindwa kufunga breki na kumgonga askari huyo na kisha kuyagonga magari mengine manne yaliyokuwa mbele yake.
Kamanda Kienya alisema katika ajali hiyo, watu wengine sita walijeruhiwa. “Wao walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Aliyeumia zaidi ni huyu askari,” alisema Kamanda Kihenya.
Alisema Polisi wanaendelea kumsaka dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria, kwani alikimbia baada ya ajali kutokea.

BONYEZA HAYA MANENO "U LIKE PAGE YETU"TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527