YANATISHA!!! TAZAMA PICHA 9 ZA MAWE YALIYOPOROMOKA NA KUUA WATU WANNE HUKO MWANZA


Hizi ni baadhi ya picha za mawe yaliyoporomoka mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Mwanza na kuua watu wanne wa familia mbili.Watu hao  walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na mawe wakiwa wamelala majira ya saa nane usiku wakati mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali pamoja na radi ilipokuwa ikinyesha.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyerere A, mabatini jijini Mwanza Hassan Maulid aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Sayi Otieno na Kwinta Kweko ambao ni mume na mke huku watoto wawili Kelfine Masalu na Emanuel Joseph wa familia ya Bw.Joseph William nao pia wakipoteza maisha baada ya chumba walichokuwa wamelala kuangukiwa na jiwe lililoporomoka kutoka juu mlimani.










Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527