JE! UNAJUA MAANA YA RANGI YA MKOJO WAKO? KAMA HAPANA,BASI SOMA DONDOO HII UJIFUNZE LEO


1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi):
Unakunywa maji mengi kupita kiasi. Ikiwezekana unashauriwa upunguze kidogo

2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo: Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha.
3. Manjano iliyo pauka:
Upo kawaida tu. Endelea kunywa maji ya kutosha

4. Njano iliyo kolea:
Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji ya kutosha.

5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali:
Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sasa.

6. Rangi ya Kahawia:
Huenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kamali hii ikiendelea.

7. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu:
Kama hujala matunda yoyote nyenye asili ya uwekundu, basi huwenda una Damu kwenye kibofu chako cha mkojo. Inaweza ikawa sio ishara mbaya. Lakini inaweza ikawa ishara ya ugojwa wa Figo, uvimbe, matatizo kwenye njia ya mkojo, au matatizo kwenye kibofu. Muone daktari haraka iwezekanavyo.

Kama unadhani Dondoo hii ni Muhimu, Gonga “SHARE” ili kuwajuza na wenzako

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527