MKE WA DR SLAA ADAIWA KUHARIBU ULAJI WA KATIBU WA GEITA ALIYETIMULIWA


Aliyekuwa katibu wa Jimbo la Geita na wilaya ya Geita Rogers Ruhega na kufukuzwa uongozi wiki jana kwa madai ya kutumia madaraka yake vibaya,ameibuka na tuhuma mzito kwa mke wa katibu mkuu wa Chadema taifa Dr.Willbroad Slaa, Josephine Mushumbusi kuwa ndiye aliyepanga mkakati wa kumuondoa madarakani ili kumuwezesha mgombea mwenzake Mutta Robert apite bila kupingwa kwasababu ni kabila moja na mwana mama huyo.

Habari zinazoenezwa kwa kasi  katika mitaa mbalimbali ya mji wa Geita na kusambazwa na wanachama wa chadema wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa Ruhega zinataja kuwa mke wa Dr.Slaa ana mahusiano ya kikabila na mgombea ukatibu wa jimbo hilo Mutta Robert kwamba ametumika kumshawishi mme wake amfukuze Rogers Ruhega ili Mutta Robert agombee peke yake bila kupingwa.

Madai hayo ya ukabila  yanakuja siku chache baada ya Katibu huyo kuandika barua kali kwa wanachama kumi kuwataka wajieleze kwanini wasivuliwe uanachama kwa madai kuwa wanaendesha siasa za kuhubiri ukabila kuwa wanapinga waha wasichaguliwe katika jimbo la Geita  bali wachaguliwe wasukuma tu.

Baada ya Mwenyekiti wa Kanda ya ziwa Magharibi Peter Mekere kumvua madaraka yote Ruhega,Propaganda za ukabila wa kisukuma zikabadilika kuwa za ukabila wa kihaya kupitia kwa mke wa Dr Slaa wakimuhusisha kumbeba mgombea ukatibu wa jimbo hilo Robert ambaye ni Mhaya.

Augosti ,14 mwaka  huu viongozi wa kanda ya ziwa magharibi walinusurika kupigwa mawe na vjana wanane waliovamia mkutano mkuu wa kata ya Kalangalala wa uchaguzi wakipinga kufanyika kwa uchaguzi huo na kusababisha mwenyekiti wa mtaa wa Tambukareli kupigwa na kujeruhiwa mdomoni kwakipigo kikali na kuripoti polisi.

Katika uchaguzi huo ambao ulikuwa unafutwa kiaina na katibu huyo mara mbili,viongozi waliokuwa wamefutwa walichaguliwa tena kwa kishindo na kurudi kwenye nafasi zao za awali kama zilivyo kwenye mabano,Charles Yatobanga(mwenyekiti),Julius Charles (katibu),Gabriel Masunga Nyasilu(katibu mwenezi),Mabula Ndoshi (mweka hazina).

Wengine ni Yukuli Ludandali (mwenyekiti Bavicha),Paul Galus (katibu bavicha),Flora Rumanyika(mwenyekiti bawacha),Batha Nchimani(katibu bawacha) na Itika Kinyahiya (mwenyekiti wazee),Wambura Mwita(katibu wazee)

Baadhi ya majina yaliyoshinda katika uchaguzi huo ni wale waliokuwa wametajwa katika mtando wa kiamii wa jamii forum iliyoandikwa na Jackton Manyerere kuwa ni wasaliti na wanatakiwa kufukuzwa uanachama kuwa wanashirikiana na mbunge wa ccm viti maalum,Vicky Kamata kuharibu chadema.

 Wakati hayo yakiendelea ,Mwandishi wetu alibahatika kumfuma moja kwa moja katibu aliyefukuzwa akichinja kuku mchana mweupe hadharani majira ya saa kumi jioni jana katika maeneo ya kampuni ya ujenzi ya Kassco jirani na nyumbani kwake kwenye vichaka kama ishara ya kutoa kafara na matambiko ya jadi.

Johnson Mutagwaba ambaye anayekiri kuwa mfuasi mwaminifu wa katibu huyo,alikiri kununua kuku huyo soko kuu la Geita mjini na kuwa yeye alidhani ni kwa matumizi ya kitoweo na kwamba kama angejua ni kwa matumizi ya matambiko asingekubali kutumwa kumunua sokoni.

Mgombea ukatibu wa jimbo la Geita Mutta Robert,alisema kuwa....

,”tuhuma zinazoelekezwa kwangu kuhusu mke wa Dr.Slaa si za kweli ni siasa za maji taka maana hata miimi sijuani na huyo mama na wala hatujawahi kukutana popote,lakini tangu mwanzo wakati nimechukua fomu ya kugombea ukatibu yaliibuka mambo mengi”

“Niliwahi kuzushiwa kuwa natukana viongozi wa chadema,na kuna watu wasiojulikana wamefikia hatua ya kufungua akaunti kwenye jamii forum  kwa majina yangu na wanaposti matusi kwa viongozi wa chadema ili kuaminisha umma kuwa mimi ndiye ninaye tukana viongozi kupitia mitandao ya kijamii”

“Kwahiyo sishangai leo nikihusishwa na mke wa Dr.Slaa maana siwezi kuzuia watu kufikiri lakini muarobani wa haya yote ni siku ya uchaguzi baada ya wapiga kura kuamua nani awe katibu wao na mimi siko tayari kushiriki siasa chafu,acha wafanye wao.

Na Victor Bariety-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527