Breaking News_ MABASI YAGONGANA NA KUUA WATU ZAIDI YA 10 HUKO TABORA


Ni katika eneo la ajali 
 Hali ni tete sana eneo la Mkolye, takribani km 4 toka Mjini Sikonge baada ya basi la Sabena lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Mwanza na basi la A.M. toka Tabora kwenda Mpanda Katavi kugongana uso kwa uso. 
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio 
Zoezi la kutoa miili ya marehemu likiendelea
Miili ya marehemu ikiwa eneo la tukio



Abiria kadhaa wakiwa wamenasa katika mabasi hayo,  



Majeruhi
Majeruhi
Majerhi
Majeruhi
Majeruhi
Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba watu zaidi ya 10 wanadaiwa kupoteza maisha papo hapo na wengine  zaidi ya 70  wajeruhiwa baada ya basi la linalofahamika kama AM linalofanya safari yake Mwanza mpaka Mpanda kugongana uso kwa uso na basi lingine la Sabena ambalo linafanya safari zake Mbeya kwenda Tabora.

Ajali hiyo imetokea leo  majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda  Mwanza kugongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri  T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda. 
Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani   Sikonge.

Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papo hapo na kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi (Day-worker)

Inaelezwa  kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibika vibaya sana.

Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la  Sabena lililokuokea  Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea  Mwanza kwenda Mpanda.

Majeruhi baadhi wakiwa wamekatika mikono na miguu,wamepelekwa katika Hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527